Pata taarifa kuu
DRC-UCHUNGUZI

DRC: Rais Tshisekedi amfuta kazi Albert Yuma kama mwenyekiti wa bodi ya GECAMINES

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi amemuachisha kazi Albert Yuma, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya GECAMINES, kampuni ya madini ya serikali.

Albert Yuma, mkurugenzi mkuu wa zamani wa GECAMINES.
Albert Yuma, mkurugenzi mkuu wa zamani wa GECAMINES. © JACQUES DEMARTHON / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu Novemba 19, uchunguzi wa Congo Hold-up umetaja jina lake mara kwa mara. Ikiwa na makumi ya mamilioni ya dola, kampuni ya madini ya serikali ilifadhili akaunti za kundi la washirika wa karibu wa Joseph Kabila, kupitia Benki ya BGFI. Pia alikuwa chini ya uchunguzi na Ukaguzi Mkuu wa Fedha.

Rais Tshisekedi amebadilisha bodi nzima ya GECAMINES akiwemo mwenyekiti wake Albert Yuma, mkurugenzi wake mkuu na naibu mkurugenzi mkuu. Ubadhirifu mwingi umeshutumiwa katika muktadha wa uchunguzi wa Congo Hold-up.

Binafsi, mkurugenzi mkuu huyo wa zamani wa GECAMINES anahusika katika kesi ya Egal, kampuni ambayo yeye ni mwanahisa na ambaye alipitisha mlango wa nyuma dola milioni 43 za pesa za umma kwa faida ya watu wa karibu wa Joseph Kabila.

Chini ya udhibiti wake, GECAMINESs ilitoa fedha nyingi na kuzihamisha kwenye akaunti za benki kama malipo ya ushuru, ikimaanisha ushuru wa siku zijazo.

Ukaguzi Mkuu wa Fedha, IGF, unasema dola nusu bilioni moja ndio pesa ambazo zilipitishwa mlango wa nyuma. Kwa sababu badala ya kulipa fedha kwenye akaunti ya hazina ya serikali, kampuni hiyo ililipa kwa akaunti ya Sud Oil, kampuni ambayo ni ya wanafamilia wa Joseph Kabila. Kwa mfano tarehe 13 Juni 2016, milioni 2 zilitoweka kwa madai kuwa ni pesa za "ushuru wa mapema".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.