Pata taarifa kuu
AFRIKA-USHIRIKIANO

Afrika-China: Nchi za Afrika zasubiri hatua baada ya ahadi za Beijing

Kongamano la 8 la Ushirikiano kati ya Afrika na China lililoandaliwa mwaka huu mjini Dakar lilimalizika Jumanne, Novemba 30. Baada ya miaka 21 ya ushirikiano kupitia shirika hili, viongozi wa Afrika walikuwa na nia ya kuweka mbele vipaumbele vyao ili kusawazisha uhusiano na Beijing. Lakini licha ya ahadi za rais wa China, hawana uhakika kwamba bara hilo litaona mabadiliko ya kweli katika muda mrefu.

Wajumbe wa Senegal wanaingia kwenye Kongamano la ushirikiano kati ya Afrika na China mjini Dakar, Novemba 30, 2021.
Wajumbe wa Senegal wanaingia kwenye Kongamano la ushirikiano kati ya Afrika na China mjini Dakar, Novemba 30, 2021. © SEYLLOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa China Xi Jinping alitoa orodha ya ahadi kwa Afrika, moja ambayo ni ya kuvutia: dozi bilioni moja za chanjo ya Covid-19. Rais wa China pia aliahidi kuwekeza dola bilioni 10 katika uwekezaji wa makampuni ya China ili kuifanya Afrika kuwa ya viwanda, dola bilioni 300 katika uagizaji wa ziada wa bidhaa za kilimo za Afrika na kufuta deni la nchi zilizoendelea kidogo zaidi kwa mwaka 2021. Kwa mtazamo wa kwanza, rais wa China alijibu kuhusu karibu hoja zote zilizotolewa mjini Dakar au kwa njia ya video na Macky Sall, rais wa Senegal, Félix Tshisekedi, rais wa DRC na Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Aïssata Tall Sall alisema ameridhishwa na kuzingatia kwa China vipaumbele vya Afrika, lakini anasubiri ahadi hizi kutimia na mabadiliko ya kweli.

[...] Tunafuraha kutambua kwamba masuala haya yamekuwa mada ya maelewano mapana kati ya Afrika na China na kwamba yamezingatiwa katika hati za kazi zilizowasilishwa kwa ajili yetu. Ni lazima sasa tukubaliane kuhusu mbinu mpya za kufanya kazi zenye ufanisi zaidi ambazo zitakuza ushirikishwaji na kasi katika utekelezaji wa programu zetu za ushirikiano ili kila mwanachama aweze kufaidika ipasavyo na kikweli kutokana na matokeo ya ushirikiano wetu.

Kwa upande wake, Thierry Pairault, mkurugenzi wa utafiti katika taasisi za CRNS na EHESS, mtaalamu wa masuala ya China-Afrika, amesema tatizo la deni la muda mrefu la Afrika halijatatuliwa, wala kutofichwa kwa mikataba ya China. Ikitokea mzozo na mataifa ya Afrika, China ambayo iliweka mahakama yake ya usuluhishi mjini Beijing, imekubali kuihamishia Hong Kong, jambo ambalo si la maendeleo.

La muhimu ni iwapo deni hilo lilitolewa kwa uhakika kwamba ulipaji wa deni ulikuwa umepangwa. Na hapa ndipo shida inapotokea ...
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.