Pata taarifa kuu
CHINA-USHIRIKIANO

Rais wa China aahidi kutoa dozi bilioni 1 za chanjo dhidi ya Covid-19

Katika siku ya kwanza ya kongamano la nane la ushirikiano kati ya China na Afrika, lililoandaliwa mjini Dakar, Rais Xi Jinping wa China amezungumza Jumatatu, Novemba 29, kwa njia ya video. Ametangaza kuwa China itaipatia Afrika dozi bilioni 1 za chanjo dhidi ya Covid-19.

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba kwa njia ya video kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mjini Dakar, Senegal, Novemba 29, 2021.
Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba kwa njia ya video kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mjini Dakar, Senegal, Novemba 29, 2021. REUTERS - COOPER INVEEN
Matangazo ya kibiashara

Dozi mpya bilioni moja za chanjo kutoka China, ikiwa ni pamoja na dozi milioni 600 ambazo ni kama msaada. Hii ndiyo ahadi ambayo Xi Jinping ameitoa kwa Afrika wakati wa sherehe za ufunguzi wa kongamano kati ya chian na Afrika mjini Dakar, ili bara hilo liweze kuchanja asilimia 60 ya wakazi wake ifikapo mwaka 2022. Kwa sasa wamefikia asilimia 6 ya Waafrika waliochanjwa.

Rais wa China pia amefurahishwa kuona nchi nyingi zaidi za Afrika zinajiunga na mpango wa Silk Road, mpango wa maendeleo ulioasisiwa na Serikali ya watu wa China. Pia aliahidi kukuza biashara kati ya Afrika na China, hususan kuongeza mauzo ya bidhaa za kilimo kutoka Afrika kwenda China hadi dola bilioni 300, ndani ya miaka mitatu, kwa kuharakisha ukaguzi wa bidhaa za Afrika na kusamehe ushuru zaidi wa bidhaa hizo.

Xi Jinping pia ameahidi kuongeza uwekezaji wa moja kwa moja wa makampuni ya China hadi zaidi ya dola bilioni 10, ili kuharakisha ukuaji wa viwanda katika bara la Afrika.

Rais wa China pia ameahidi kupunguza deni la nchi zilizoendelea kidogo zaidi za Afrika, kuelekea China ambayo ni mkopeshaji mkuu wa bara hilo.

Mkutano huo ulmeanza Jumatatu asubuhi baada ya mkutano wa kiwaziri wa wajasiriamali kutoka China na Afrika, fursa kwa pande hizo mbili kujadili ushirikiano huu wa China na Afrika uliopunguzwa kasi kutokana na janga la Covid-19, lakini ambalo kwa hakika linaanza tena.

Uwekezaji umeanza tena na katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka huu wa 2021 pekee, China imewekeza dola bilioni 2.5 barani Afrika, kulingana na Makamu wa Waziri wa Biashara wa China ambaye alizungumza kwa njia ya video.

Katika nyanja ya kijamii, China imeipatia Afrika dozi milioni 160 za chanjo dhidi ya Covid-19 na itaendelea, kulingana na makamu wa waziri wa biashara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.