Pata taarifa kuu
DRC-MIUNDOMBINU

Wasiwasi wa kutomalizika kwa miundo mbinu muhimu mjini Lubumbashi

Ni miaka 11 sasa tangu serikali ya DRC iliposaini mkataba na makampuni ya China, huku serikali nchini humo ikiwapa shamba la madini na kampuni hizo za China kuahidi kukarabati na kujenga upya  miundo mbinu ya reli na barabarabra kwa Dola Bilioni Sita, lakini mpaka sasa mengi hajafanyika.

Kiwanda cha cobalt mjini  Lubumbashi, Kusini Mashariki mwa DRC.
Kiwanda cha cobalt mjini Lubumbashi, Kusini Mashariki mwa DRC. SAMIR TOUNSI AFP
Matangazo ya kibiashara

Pembezoni mwa soko la Kenya mjini Lubumbashi Lwembo wa Nsenga anafatilia upakiaji wa mizogo ndani ya lori lake kusafiri umbali wa Kilomita 900 kati ya Luambo–Mitwaba–Manono.

Mpaka sasa ni umbali tu wa Kilomita 100 ya barabra ya udongo ndiyo iliyokarabatiwa.

Kutoka Lubumbashi mpala Kyolo ni Kilomita 566 na hapo unasafiri kwa muda wa siku mbili, ukijaribu kupita gari linakwama kwa sababu barabara ni mbaya sana.

Kazi ya ukarabati wa miundo mbinu iliyoanza mwaka 2014, baada ya makubaliano ya nchi hizo mbili, ilileta matumaini makubwa, lakini matumaini ya kukamilika hivi karibuni, yanaonekana kuvunja moyo.

Erick Lubamba Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Lubumbashi anaona kuwa, bado kuna kazi kubwa kumaliza kazi hiyo.

Hapa Lubumbashi, barabara ya Kasavubu iliboreshwa lakini kwas asa hivi, kazi hiyo imeanza upya hii inamaana kuwa hakuna faida ya pesa zilizotumiwa.

Hadi sasa,  sehemu ya miundombinu ya mpango huo wa Sino Congolais, umeipa DRC kiasia cha mkopo wa zaidi ya Dola Bilioni 2.8 lakini Shirika la  AFREWATCH linaona kuwa hii italiongezea deni nchi hiyo.

Emmanuel Umpula , kiongozi wa shirika hilo, anasema;

Kufikia mwaka 2017, Congo imelipa kampuni ya  Sicomines kiwango cha  Dola Milioni  Themanini na tatu na kampuni hii haijapata faida ili kuruhu ulipahi wa deni. Kampuni hiyo imefanikiwa tu kuzalisha toni Elfu Tisini na tano ya shaba licha ya kutakiwa kutoa tani Laki nane ya shaba.

Upande wake, makamo kiongozi wa mpango  SinoCongolais akiwa jijini Kinshasa anasema,  mamilioni ya Dola imetolewa kufadhili miradi zaidi ya arobaini nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.