Pata taarifa kuu
CHINA-USHIRIKIANO

China na Afrika: Serikali za Afrika zataka kuwepo kwa uhusiano wenye uwiano zaidi

Kongamano la Ushirikiano kati ya China na Afrika linaendelea mjini Dakar. Mawaziri kadhaa wa China wanashiriki mkutano huu. Sehemu muhimu ya mijadala katika kongamano hili inahusu uhusiano wa kiuchumi kati ya China na bara la Afrika. Beijing inasalia kuwa mshirika mkuu wa kibiashara wa bara hili. Lakini uhusiano huu hauna usawa na leo wakuu wa nchi za Kiafrika wanataka kubadilisha hali hiyo.

Rais wa Senegal Macky Sall akizungumza katika Kongamano la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) mjini Dakar, Novemba 29, 2021.
Rais wa Senegal Macky Sall akizungumza katika Kongamano la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) mjini Dakar, Novemba 29, 2021. AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Katika siku ya kwanza ya kongamano la nane la ushirikiano kati ya China na Afrika, lililoandaliwa mjini Dakar, Rais Xi Jinping wa China amezungumza Jumatatu, Novemba 29, kwa njia ya video. Ametangaza kuwa China itaipatia Afrika dozi bilioni 1 za chanjo dhidi ya Covid-19.

Mnamo 2019, biashara kati ya China na Afrika ilifikia karibu dola bilioni 210. Katika mwaka huo huo, nakisi ya kibiashara ya mataifa ya Afrika ukilinganisha na China iliongezeka mara tatu, na kufikia karibu dola bilioni 18. Ni wazi, China inasafirisha bidhaa nyingi zaidi barani Afrika kuliko inavyoagiza kutoka nje. Aidha, inasafirisha bidhaa za viwandani zilizoongezwa thamani ya juu, huku ikiagiza zaidi malighafi kutoka nje.

Hali isiyo na usawa ambayo inapaswa kubadilishwa, kulingana na Macky Sall, rais wa Senegal. “Lazima tuharakishe maendeleo ya uwezo wa kiviwanda barani Afrika ili bara hili liweze kurahisisha upatikanaji wa bidhaa zake kwenye soko la China. Aidha, upatikanaji bora wa bidhaa za Kiafrika kwenye majukwaa ya kielektroniki ya China ungesaidia kuongeza kiwango cha biashara yetu kwa manufaa ya pande zote mbili. "

Maombi ambayo Rais wa China Xi Jinping anasema aliyasikia. "China itapanua aina za bidhaa zinazonufaika kutokana na msamaha wa ushuru kwa nchi zenye maendeleo duni ili kuleta jumla ya bidhaa zinazoagizwa na China kutoka Afrika hadi dola za Marekani bilioni 300 katika miaka mitatu ijayo. "

Ingawa 70% ya mauzo ya nje ya Afrika yanaelekezwa China, mnamo mwaka 2019 yaliwakilisha 4% tu ya usawa wa biashara ya China.

Tatizo la uhusiano kati ya China na Afrika ni kwamba kulikuwa na kukosekana kwa usawa, kama ilivyoshuhudiwa hatu kwa hatua kwa miaka mingi kati ya China na nchi za Afrika, na hapo wazo ni kujibu maswali yanayoibuka juu ya faida ipi kwa Waafrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.