Pata taarifa kuu
MISRI-HAKI

Ishirini na mbili wahukumiwa adhabu ya kifo baada ya kupatikana na hatia Misri

Misri imewahukumu kifo watu 22 kwa tuhuma ya kupatikana na hatia ya kutekeleza mashambulizi 54, ikiwemo jaribio la kumuua aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, Mohamed Ibrahim.

Misri imekuwa ikipambana na makundi ya kijihadi eneo la Kaskazini mwa Sinai, tangu kuondolewa madarakani kwa rais Mohamed Morsi mwaka 2013, hali iliolazimu jeshi na polisi kuanzisha operesheni kali eneo la Sinai mwaka 2018.
Misri imekuwa ikipambana na makundi ya kijihadi eneo la Kaskazini mwa Sinai, tangu kuondolewa madarakani kwa rais Mohamed Morsi mwaka 2013, hali iliolazimu jeshi na polisi kuanzisha operesheni kali eneo la Sinai mwaka 2018. © RFI/Véronique Gaymard
Matangazo ya kibiashara

Raia hao 22, akiwemo afisa wa polisi wamehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya  kutekeleza mashambulizi 54 ya kigaidi kote nchini Misri pamoja na jaribio la mauwaji dhidi ya waziri Ibrahim.

Ni hukumu ambayo imetolewa baada ya watu hao 22 kupatikana kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Ansar Beit al-Maqdis, ambalo lina uhusiano na kundi la Islamic State.

Hukumu ya kifo nchini Misri hutekelezwa kwa kuwanyoga wahusika, na haina rufaa, Mahakama ya juu zaidi nchini Misri pia imedumisha uamuzi wa awali wa kuwafunga kifungo cha maisha washukiwa wengine 118 katika kesi hiyo.

Misri imekuwa ikipambana na makundi ya kijihadi eneo la Kaskazini mwa Sinai, tangu kuondolewa madarakani kwa rais Mohamed Morsi mwaka 2013, hali iliolazimu jeshi na polisi kuanzisha operesheni kali eneo la Sinai mwaka 2018.

Zaidi ya washukiwa wa makundi ya kijahadi 1,073, wameuawa tangu mwaka 2018, Misri na Isreali mapema mwaka huu zikikubaliana kushirikiana ili kumaliza makundi ya kijihadi eneo la Rafah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.