Pata taarifa kuu
SUDAN-HAKI

Kiongozi wa Al Jazeera nchini Sudan aachiliwa huru baada ya siku 2 kizuizini

Mkuu wa ofisi ya Kituo cha habari cha Qatar cha Al-Jazeera mjini Khartoum, Al-Moussalami al-Kabbachi, ameachiliwa huru Jumanne hiii, kituo cha Qatar kimeripoti, huku mamia ya watu wakikamatwa tangu mapinduzi ya Oktoba 25 katika nchi hii ya Afrika Mashariki.

Vikosi vya usalama vya Sudan vikitumwa katika mji mkuu Khartoum Oktoba 25, 2021.
Vikosi vya usalama vya Sudan vikitumwa katika mji mkuu Khartoum Oktoba 25, 2021. - AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kukamatwa Jumapili nyumbani kwake, Bw. Kabbachi alipelekwa gerezani ingawa "upande wa mashtaka ulikuwa umeamuru aachiliwe", kulingana na kituo ch habari cha Al-Jazeera, kabla ya kuachiliwa hatimaye Jumanne.

"Jeshi bado halijatangaza sababu ya kuzuiliwa kwake," imesema Al-Jazeera, huku mhariri wa Gazeti la kila siku la jeshi akimshutumu Jumanne kwa "kuchapisha habari za uwongo na video za zamani "na kuwaalika" watu viongozi wanaoikosoa serikali kuchochea uhasama ".

Mamlaka mpya iliyowekwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane mara kwa mara hubatilisha maamuzi ya mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.