Sudan: Watu kadhaa wafariki dunia wakati wa maandamano ya kuunga mkono demokrasia
Katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, maandamano mapya ya kuunga mkono demokrasia yamefanyika Jumamosi hii, Novemba 13, wiki tatu baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.
Imechapishwa:
Hali ni ya wasiwasi katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum, huku watu watano miongoni mwa waandamanji wakiripotiwa kufariki dunia.
Waandamanaji wengine wameuawa mjini Khartoum siku ya Jumamosi, na kufikisha idadi ya watu watano kutoka kambi ya upinzani wa mapinduzi waliouawa kwa kupigwa risasi na kurushiwa mabomu ya machozi na vikosi vya usalama, chama cha madaktari wanaounga mkono demokrasia umesema.
Makumi kwa maelfu ya Wasudan wanaendelea kupiga kelele "Hapana kwa utawala wa kijeshi" katika mitaa ya Khartoum na miji mingi nchini Sudan wakati wa maandamano nchini Sudan dhidi ya mapinduzi yaliyoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane.
"Watu wengi wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi katika maeneo tofauti ya Khartoum", chama cha madaktari wanaounga mkono demokrasia kimeongeza.
Inarifiwa kuwa takriban waandamanaji 20 wameuawa tangu Oktoba 25.
Kisa cha urushaji wa gesi ya kutoa machozi kimeripotiwa huko Omdurman, magharibi mwa Khartoum.