Pata taarifa kuu
SUDAN-USALAMA

Sudan: Mvutano waendelea kujitokeza kati ya raia na wanajeshi

Baada ya maandamano ya Jumamosi, Novemba 13, yaliyokandamizwa na kusababisha vifo vingi, mvutano kati ya raia na wanajeshi nchini Sudan unaendelea. Hii inatatiza zaidi upatanishi unaofanywa katika jaribio la kuirejesha nchi hiyo kwenye taasisi za kidemokrasia za mpito.

Waandamanaji katika mitaa ya Khartoum Novemba 14, 2021.
Waandamanaji katika mitaa ya Khartoum Novemba 14, 2021. AP - Marwan Ali
Matangazo ya kibiashara

"Ukandamizaji wa umwagaji damu siku ya Jumamosi ni uthibitisho kwamba Jenerali Burhan hajadhamiria kutafuta suluhu la mgogoro," amesema kijana mmoja, raia wa Sudan, aliyeshiriki katika mtandao wa kamati za upinzani Jumamosi mchana. Kwa hivyo, kambi hii inayopinga mapinduzi unakusudia kuzidisha shinikizo na tayari wanataka kufanyikakwa maandamano mapya Jumatano, Novemba 17.

Kwa upande wa jeshi, na wakati waandamanaji wanaendelea kuhesabu idadi ya vifo, jana Jenerali Burhan aliongoza mkutano wa kwanza wa baraza jipya la uhuru. Uteuzi wa baraza hili jipya umeelezewa na Umoja wa Mataifa kama wa "upande mmoja," na kuonekana na wengi kama njia ya mkuu wa jeshi kuidhinisha mapinduzi yake.

Wakati huo huo, operesheni ya kamata kamata inaendelea katika maeneo mbalimbali na katika taasisi za umma wapinzani wa mapinduzi, wamekuwa wakichukuliwa na fasi zao na maafisa wa serikali ya zamani.

"Kambi hizi mbili zinazidi kuwa na mgawanyiko," amebaini mtafiti wa Sudan Kholood Khair. Hii inaweza kuhatarisha zaidi kazi ya wale ambao, wamekuwa wakijaribu tangu Oktoba 25 kupatanisha raia na askari na kuokoa taasisi za kidemokrasia za mpito.

Moja ya gari la kubebea wagonjwa lililotumika kuwasafirisha walioshambuliwa. Walirusha mabomu ya machozi, vifaa vikaharibika ... ingawa ni gari la wagonjwa la serikali.

Hospitali za Khartoum zimezidiwa na wingi wa wagonjwa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.