Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-AKI

Kesi ya mauaji ya Sankara: Kanali Jean-Pierre Palm afikishwa kizimbani

Nchini Burkina Faso, kesi ya wanaodaiwa kumuua Thomas Sankara inaendelea mbele ya mahakama ya kijeshi huko Ouagadougou.

Watu wanahudhuria ufunguzi wa kesi ya wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya Thomas Sankara huko Ouagadougou Oktoba 11, 2021.
Watu wanahudhuria ufunguzi wa kesi ya wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya Thomas Sankara huko Ouagadougou Oktoba 11, 2021. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu hii, Novemba 8, mshtakiwa Jean-Pierre Palm, mkurugenzi wa zamani wa usalama wa kitaifa, aliteuliwa kuwa mkuu wa vikosi vya ulinzi mwezi mmoja baada ya mapinduzi, bado amefikishwa kizimbani na kusikilizwa na majaji. Katika kusikilizwa pia, kimemtia hatiani rais wa zamani Blaise Compaoré.

Jean-Pierre Palm anatuhumiwa kushiriki katika kuhatarisha usalama wa nchi. Muda mfupi kabla ya mapinduzi, alikuwa mkuu wa idara ya upelelezi.

Suala la Jumatatu asubuhi lilikuwa iwapo alijua kuhusu jaribio la mapinduzi, kwa kiwango gani, na kama alikuwa alihusika kwa njia moja ama nyingine. Kwa upande wa mshtakiwa, amesema ukweli ni kwamba: hakujua chochote, alikuwa kwa daktari wa meno wakati serikali iliposhambuliwa, basi, katika msukosuko huo, alialikimbilia kwa mtu anayemjua, ilikuwa usiku na siku iliyofuata alienda kwa kwenye makao makuu ya serikali na kupata habari juu ya kifo cha Thomas Sankara.

“Wewe ni mwanajeshi, ulisimamia ulinzi, unasikia milio ya risasi na unakimbilia kwa rafiki yako kwa sababu huelewi kinachoendelea? ", Ameshangaa Ferdinand Nzepa, wakili wa familia ya Sankara.

"Ulitaka nifanye nini?" Nilikuwa peke yangu, nimevaa kiraia na bila silaha, "alijibu Jean-Pierre Palm.

Jean-Pierre Palm anashukiwa kuharibu, siku moja baada ya Oktoba 15, 1987, mitambo ya kurekodi sauti ya vikosi vya ulinzi akishirikiana na maafisa wa Ufaransa. Inashukiwa kwamba wakati huo, washirika wa Thomas Sankara walikuwa walirekedi sauti za viongozi kadhaa ikiwa ni pamoja na Blaise Compaoré, na rekodi hizi kwa hiyo zingeweza kumtia hatiani rais huyo wa zamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.