Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Watu 13 wauawa katika makabiliano ya jamii mbili hasimu magharibi mwa DRC

Watu 13 wameuawa, na wengine kadhaa kujeruhiwa na karibu nyumba hamsini zimeteketezwa kwa moto katika mapigano kati ya jamii mbili zinazopigania ardhi kaskazini magharibi mwa DRC.

Mwanajeshi la DRC amesimama karibu na jengo lililoteketezwa katika mji wa magharibi wa Yumbi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Februari 1, 2019.
Mwanajeshi la DRC amesimama karibu na jengo lililoteketezwa katika mji wa magharibi wa Yumbi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Februari 1, 2019. ALEXIS HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mkuu wa wilaya ya Kungu katika mkoa wa Sud-Ubangi, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo Jean- Pierre Elongo, amesema kuwa mzozo wa ardhi ndio chanzo cha mapigano hayo yaliyogharimu maisha ya watu kumi na watatu na nyumba kadhaa kuteketezwa.

Elongo amesema mzozo wa ardhi kati ya jamii hizo mbili umedumu tangu mwaka 1982 bila ya kufikia makubaliano na kwamba serikali ya eneo hilo inajaribu kuzipatanisha pande hizo hasimu bila mafanikio.

Mapigano hayo yaliyodumu siku tatu tangu siku ya Jumatatu hadi Jumatano wiki hii yaliyahusisha makundi ya watu waishio eneo la Lingotebe na Kungu, ambapo wakuu wa serikali wanasema hadi sasa miili ya watu 13 waliouawa kwa kuchomwa visu ndio ilipatikana huku kukiwa, majeruhi kadhaa na karibu nyumba hamsini zimeteketezwa kwa moto, maafisa wa usalama wamebainisha hapo siku ya Alhamisi.

Eneo la Kungu liko karibu kilomita mia moja kutoka mji wa Gemena, mji mkuu wa mkoa wa Sud-Ubangi. Mwaka 2010, ulizuka mzozo mwengine kati ya jamii ya Muzaya na Enyele ambao walikuwa wanapigania udhibiti wa mabwawa huko Ubangi ya Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.