Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Raia wa Beni waendelea kukabiliwa na madhila mbalimbali kutoka waasi wa ADF

Waasi wanaodaiwa kuwa wa ADF wamewauwa watu wanane na kuwateka wengine baada ya kushambulia vijiji vya Mbingi na Mapasana, mwishoni mwa wiki iliyopita, Wilayani Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Vikosi vya jeshi la DRC, FARDC wakiendelea kukabiliana na makundi ya waasi mashariki mwa DRC.
Vikosi vya jeshi la DRC, FARDC wakiendelea kukabiliana na makundi ya waasi mashariki mwa DRC. © AFP PHOTO / Alain WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

Mbali na mauaji hayo, waasi hao waliteketeza moto makaazi ya watu, huku waliouawa wakipigwa risasi au kukatwa shingo.

Mauji kama haya yameendelea kushuhudiwa Wilayani Beni, licha ya mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri kuwa chini ya uongozi wa kijeshi tangu mwezi Mei, ili kupambana na utovu wa usalama, Mashariki mwa nchi hiyo.

Waasi kutoka Uganda ADF wanazidisha mashambulizi yao dhidi ya vijiji mbalimbali huku wakiwauwa raia wengi.

Kwa kipindi cha wiki moja, waasi kutoka Uganda ADF, wamewaua raia karibia mia mbili, katika mashambulizi mbalimbali yaliyolenga vijiji kwenye wilaya ya Beni, hasa katika sekta ya Ruwenzori mkoani Kivu ya Kaskazini, na pia katika vijiji vya Boga na Tchabi, katika wilaya ya Irumu mkoani Ituri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.