Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

HRW: Raia 740 wauawa tangu kutangazwa kwa sheria ya kijeshi mashariki ma DRC

Mashambulio ya makundi yenye silaha dhidi ya raia yameendelea katika mikoa inayokumbwa na mizozo ya Ituri na Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tangu serikali kutangaza sheria ya kijeshi mwezi Mei 2021, shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema kwenye wavuti yake.

Mmoja wa wapiganaji wa FRPI akifanya doria kusini mwa Ituri Julai 26, 2006.
Mmoja wa wapiganaji wa FRPI akifanya doria kusini mwa Ituri Julai 26, 2006. AFP PHOTO / LIONEL HEALING
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na takwimu zilizokusanywa na taasisi ya Usalama wa Kivu, mpango wa pamoja wa Human Rights Watch na Kundi la Utafiti la Kongo, tangukuanza kutekelezwa kwa sheria ya kijeshi Mei 6 hadi Septemba 10, makundi mbalimbali yenye silaha - ambayo mengine hayajulikani - yaliua angalau raia 672 na vikosi vya usalama vya DRC viliua raia wengine 67, katika majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini.

Moja ya mauaji mengi mnamo Agosti, HRW inaendelea, inaonyesha ukosefu wa usalama unaoendelea katika mkoa huo na majibu duni ya jeshi.

Mnamo Agosti 2, kundi la waasi wa Allied Democratic Forces (ADF), kutoka Uganda, liliripotiwa kuua raia wasiopungua 16, wakiwemo wanawake wawili, katika kijiji cha Idohu, katika jimbo la Ituri.

Makundi mingine yenye silaha na wanajeshi wa DRC pia wamehusishwa na mashambulio katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.