Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

DRC: Wawakilishi wa dini washindwa kukubaliana juu ya mwenyekiti mpya wa CENI

Muda wa mwisho uliyotolewa na Spika Bunge la kitaifa kwa dini mbalimbali kuteua wajumbe wao kwa ofisi kuu na kamati kuu ya tume ya uchaguzi. Madhehebu sita ya kidini kati ya nane yanata Denis Kadima kuteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa CENI.

Kiongozi wa Kanisa la Uamsho nchini Congo akiwasilisha jina la mgombea aliyechaguliwa na madhehebu sita ya kidini kati ya manane katika ofisi ya CENI, huko Kinshasa, Julai 30, 2021.
Kiongozi wa Kanisa la Uamsho nchini Congo akiwasilisha jina la mgombea aliyechaguliwa na madhehebu sita ya kidini kati ya manane katika ofisi ya CENI, huko Kinshasa, Julai 30, 2021. © RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Uwaniaji wa mtaalam huyu wa uchaguzi uliowasilishwa na Kanisa la Kimbanguist unakataliwa na kanisa Katoliki na Protestanti. Madhehebu haya mawili yanaamini kwamba Denis Kadima yuko karibu sana na viongozi serikalini nchini. Kwa sasa spika wa bunge la kitaifa ndiye mwenye majukumu.

Wawakilishi wa kanisa Katoliki na Protestanti walikutana Jumatatu kabla ya saa sita mchana katika makao makuu ya Baraza Kuu la Maaskofu nchini DRC (Cenco. Hata bila wawakilishi kutoka madhehebu mengine sita, wawakilishi kutoka dini hizi mbili walikutana kwa masaa mawili na kutoa ripoti.

Katika waraka huu, wanaona kuendelea kwa utofauti, lakini wanasema bado wako tayari kwa majadiliano zaidi ya kufunga faili hii. Cenco na ECC waliomba Jumamosi ya wiki iliyopita dini zingine zingine sita kuwasilisha mgombea mwengine tofauti na Denis Kadima.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumatatu, madhehebu hayo sita yalithibitisha msimamo wao. "Tumekubaliana kwa jambo moja kwamba mgombea wetu ni mmoja tu, Denis Kadima," amebaini Askofu Dodo Kamba, kiongozi wa Kanisa la Uamsho wa Congo.

Kutokana na hali hiyo, madhehebu hayo sita ya kidini yamemuomba spika wa Bunge kuzingatia ripoti yao na kumaliza ujumbe uliokabidhiwa wakuu wa Kanisa juu ya uteuzi wa mwenyekiti mpya wa CENI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.