Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Watoto milioni moja wa Nigeria kukosa shule kwa sababu ya ukosefu wa usalama

Watoto milioni moja nchini Nigeria wako katika hatari ya kutoweza kwenda shule kwa sababu ya tishio la ghasia, baada ya visa vingi vya utekaji nyara na mashambulizi kwa wanafunzi mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (UNICEF) lilisema Jumatano wiki hii.

Wanafunzi waliotekwa nyara na magenge ya wahalifu kaskazini magharibi na majimbo ya kati ya nchi, wengi waliachiliwa baada ya mazungumzo na kulipa fidia, baada ya wiki au miezi wakishikiliwa mateka, katika mazingira magumu, katika kambi za vijijini.
Wanafunzi waliotekwa nyara na magenge ya wahalifu kaskazini magharibi na majimbo ya kati ya nchi, wengi waliachiliwa baada ya mazungumzo na kulipa fidia, baada ya wiki au miezi wakishikiliwa mateka, katika mazingira magumu, katika kambi za vijijini. AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watoto milioni 37 wa Nigeria wanatakiwa kuanza mwaka mpya wa shule mwezi huu, lakini "mwaka huu karibu watoto milioni moja hawatakwenda shule kwani ukosefu wa usalama unatishia usalama wao na elimu," Mwakilishi wa UNICEF ​​nchini Nigeria , Peter Hawkins, alisema katika taarifa.

Kulingana na UNICEF, mashambulio 20 dhidi ya shule yaliripotiwa nchini Nigeria mwaka huu, zaidi ya wanafunzi 1,400 wametekwa nyara na 16 walifariki dunia.

Wanafunzi waliotekwa nyara na magenge ya wahalifu kaskazini magharibi na majimbo ya kati ya nchi, wengi waliachiliwa baada ya mazungumzo na kulipa fidia, baada ya wiki au miezi wakishikiliwa mateka, katika mazingira magumu, katika kambi za vijijini.

Karibu wanafunzi 200 bado hawajapatikana.

"Familia na jamii zinaendelea kuhofia kurudisha watoto zao kwenye madarasa kutokana na wimbi la mashambulio dhidi yaΒ  shule na visa vya utekaji nyara," kulingana na UNICEF.

Baadhi ya serikali za majimbo zimefunga shule kwa muda baada ya visa vya utekaji nyara.

Kwa muda mrefu majimbo ya kaskazini magharibi na kati ya nchi yamekumbwa na vurugu kati ya jamii za walimaji na wafugaji wanaohama hama ambao wanapigania ardhi na maji.

Mashambulio yamekithiri na kuibuka kwa magenge ya wahalifu walio na silaha nyingi, wanaojulikana kama majambazi, ambao hupora vijiji, huiba mifugo na kuteka nyara wakitaka fidia.

Karibu wanafunzi 70 waliotekwa nyara karibu wiki mbili zilizopita waliachiliwa wiki hii katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa nchi, ambapo jeshi limeanzisha shambulio dhidi ya magenge ya watekaji nyara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.