Pata taarifa kuu
CHAD-USHIRIKIANO

Chad yatafuta msaada wa kifedha kutoka Qatar

Rais wa Baraza la Jeshi la Chad Mahamat Idris Déby anatarajiwa kusafiri kwenda Qatar Jumapili hii kwa ziara ya siku kadhaa. Jenerali Mahamat Idris Déby anatarajia kukutana kwa mazungumzo na Emir Tamin Ben Hamad Al-Thani.

Jenerali Mahamat Idriss Deby, rais wa Baraza la Jeshi la Mpito, anatarajia kufanya ziara nchini Qatar kwa ziara rasmi kuanzia Jumapili hii, Septemba 12.
Jenerali Mahamat Idriss Deby, rais wa Baraza la Jeshi la Mpito, anatarajia kufanya ziara nchini Qatar kwa ziara rasmi kuanzia Jumapili hii, Septemba 12. AFP - BRAHIM ADJI
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri kadhaa tayari wako Doha kwa mazungumzo. Chad inategemea Qatar kuisaidia kifedha, lakini pia inaweza kuchukua jukumu katika mchakato wa kisiasa.

Miongoni mwa mawaziri ambao tayari wako Doha, ni Chérif Mahamat Zène, Waziri wa Mambo ya Nje, na yule wa fedha, Tahir Hamid, wamekuwa wakifanya mazungumzo tangu siku ya Alhamisi.

Sehemu ya kwanza ya ziara hii ni ya kiuchumi: Chad inahitaji pesa kufadhili gharama za kipindi cha mpito na mazungumzo ya kitaifa. Kitita ambacho serikali inahitaji ni Faranga za CFA bilioni 841, sawa na euro bilioni 1.3.

Hata hivyo, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF)wiki hii uliwataka wadai binafsi wa nchi hiyo kushiriki katika urekebishaji wa deni, na Qatar ni mwanahisa mkubwa wa Glencore, kampuni ya Uswisi ya madini ambayo inamiliki visima vya mafuta nchini Chad, na inaongoza kundi la wakopeshaji ambalo Ndjamena inadaiwa zaidi ya euro bilioni 1.

Suala lingine, ambalo ni lile la majadiliano na makundi ya kisiasa yenye silaha. Kiongozi wa kundi la waasi la UFR Timan Erdimi, anaishi Qatar tangu mwaka 2009. Kulingana na kiongozi wa kundi hilo,  na kulingana na afisa wa Chad, hakuna mawasiliano yoyote yaliyofanyika kwa sasa.

Hata hivyo, Mahamat Idriss Déby ameahidi kuendelea kwenye njia ya maridhiano, na amefanya siku kadhaa huko Amdjarass, mashariki mwa nchi. Ni ngome ya jamii ya Zaghawa ambayo wawili hao, ambao ni binamu, wanatoka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.