Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Kinshasa yasihi raia wake kutokuwa na wasiwasi juu jeshi la Uganda kuingia DRC

Rais wa Uganda Yoweri Museveni Jumatano (Septemba 8) alisisitiza nia yake ya kuingilia kijeshi mashariki mwa DRC ili kupigana na waasi wa ADF kutoka Uganda. Alibaini kwamba majadiliano yanaendelea na Kinshasa kuhusu suala hilo. Nchini DRC, tangazo hilo limechukuliwa kuwa halina uzito wowote.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni. via REUTERS - PRESIDENTIAL PRESS SERVICE
Matangazo ya kibiashara

Mbunge Juvenal Munubo, mjumbe wa kamati ya Bunge husu masuala ya ulinzi na usalama, ni miongoni mwa wa kwanza kusema juu ya matamshi ya rais wa Uganda aliyehojiwa na wenzetu wa France 24. Anaona kuwa mazingira hayaruhusu na kukumbusha kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Haki ililaani Uganda kwa ukiukaji wa sheria za nchi ya DRC na ukiukaji wa haki za binadamu ilipoingiliakijeshi nchini DRC kati ya 1998 na 2003.

Amebaini kwamba inatosha tu kuishia kwenye kupeana taarifa za kijasusi na Uganda kama nchi zingine jirani. Badala yake, anaomba suluhisho la ndani na kutaka jeshi la DRC kupewa uwezo wa kutosha kutokomeza makundi yenye silaha nchini humoikiwa ni pamoja na ADF na vile vileΒ  kuboresha uhusiano kati ya raia na jeshi.

Kwa upande wake, mdau wa kimataifa Martin Ziakwau Lembisa amebaini kwamba wapiganaji wa ADFwanashirikiana na baadhi ya wanamgambo wa Mai-Mai kwa kutekeleza maovu yao.

Mamlaka ya DR Congo inasema kuwa kufikia hatua hii ni suala tu la kupeana taarifa za kijasusi. Kwanza katika ngazi ya kikanda, kupitia Jumuiya ya Maziwa Makuu, hasa kupitia makubaliano yanayoitwa Mkataba wa Nairobi uliosainiwa mnamo 2006; kisha kwa pamoja - mkutano wa mwisho wa ngazi ya juu kati ya nchi hizo mbili uliyofanyika Beni miezi miwili iliyopita.

Museveni ajitetea

Yoweri Museveni, akihojiwa kuhusu ugaidi nchini Msumbiji, alihakikisha kwamba chanzo cha tatizo hilo kiko kwa jirani yake, DRC: β€œTatizo la Msumbiji linahusiana na tatizo mashariki mwa DRC. Magaidi hawa nchini Msumbiji wamepitia DRC katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita. Tatizo la DRC lazima litatuliwe na lile la Msumbiji. Na tuko tayari kuchangia wakati wowote. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.