Pata taarifa kuu
UGANDA-ULINZI

Uganda kutuma wanajeshi mashariki mwa DRC kupambana na ADF

Waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) ni kundi la waasi wenye silaha wenye asili ya Uganda. Wameshutumiwa kwa mauaji mengi kwa karibu miaka saba katika eneo la Beni lakini pia katika mkoa wa Ituri, mashariki mwa DRC, mpakani na Uganda.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi (kushoto) akipokelewa na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni, huko Entebbe, Novemba 9, 2019.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi (kushoto) akipokelewa na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni, huko Entebbe, Novemba 9, 2019. Sumy Sadurni / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, alizungumza na wenzetu kutoka France 24 Jumatano tarehe 8 Septemba. Aliahakikishia kuwa majadiliano yanaendelea na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi Tshilombo.

Yoweri Museveni, akihojiwa kuhusu ugaidi nchini Msumbiji, alihakikisha kwamba chanzo cha tatizo hilo kiko kwa jirani yake, DRC: “Tatizo la Msumbiji linahusiana na tatizo mashariki mwa DRC. Magaidi hawa nchini Msumbiji wamepitia DRC katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita. Tatizo la DRC lazima litatuliwe na lile la Msumbiji. Na tuko tayari kuchangia wakati wowote. "

Kama Waislam wa Ansar al-Sunna huko Msumbiji, ADF imeahidi kujiunga na kundi la Islamic State, ambalo linadai kuhusika na mashambulio mashariki mwa DRC. Katika ripoti yake ya mwisho, jopo la wataalam wa Umoja wa Mataifa lilisema hakuna uungwaji mkono wowote wa wazi wa ISIS. Bila kujali, Yoweri Museveni, anasema yuko tayari kuingilia kijeshi kwa jirani yake. Walakini, wakati France 24 ilimuuliza ikiwa rais Tshisekedi alimuomba aingilie kati, alikwepa swali akasema: "Tunazungumza suala hilo. Je! mko tayari kwa uamuzi kama huo? Majukumu haya ni ya serikali, lakini tunajadili suala hilo na rais Tshisekedi. "

Kwa upande wa DRC, inafahamika kuwa kuna ushirikiano wa kijeshi na jeshi la Uganda na majadiliano juu ya uongozi wa kiutendaji wa pamoja. Lakini kwa upande wa Kinshasa, hawajatangaza rasmi, ikiwa kuna wanajeshi wa Uganda kwenye ardhi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.