Pata taarifa kuu

Rais wa DRC, Felix Tshisekedi aelekea kumaliza ziara yake mashariki mwa nchi hiyo.

Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi, anaelekea kutamatisha ziara yake mashariki mwa nchi hiyo, ambapo amerejea mjini Goma, ambako alianzia ziara yake juma lililopita, hata hivyo ikulu ya rais jijini Kinshasa haijatoa tarifa kamili kuhusu ziara hii ya pili mfululizo kwenye mji huo wa Goma ambao hivi karibuni ulikumbwa na janga la mlipuko wa mlima wa volkano Nyiragongo.

Rais Felix Tshisekedi akiandamana na mkewe Denise Nyakeru Tshisekedi wakati wa ziara yake mjini Goma, juni 14 2021, kabla ya kuenda Beni kesho yake.
Rais Felix Tshisekedi akiandamana na mkewe Denise Nyakeru Tshisekedi wakati wa ziara yake mjini Goma, juni 14 2021, kabla ya kuenda Beni kesho yake. AFP - GUERCHOM NDEBO
Matangazo ya kibiashara

Akiwa mjini Bunia na Ituri, rais Tshisekedi aliahidi kumarishwa kwa hali ya usalama, akiapa kuyasambaratisha makundi ya waasi ambayo yamekuwa yakiwauwa watu wasio na hatia mashariki mwa nchi hiyo.

Kwenye mji wa Goma, rais Tshisekedi aliahidi kuwajengea nyumba na kuwasaidia raia ambao waliathiriwa na mlipuko wa volcano ya mlima Nyiragongo.

Wakati wa ziara yake kwenye mji wa Beni, rais Tshisekedi alishangazwa na hali ya binadamu wanaoishi katika mazingira ya hofu kufuatia mauaji yanayotekelezwa na waasi wa ADF, ambapo kiongozi huyo alisema hakuna uwezekano wowote wa kufanya mazungumzo na waasi hao.

Mbunge wa bunge la taifa Patrick Munyomo ambaye alichaguliwa katika mji wa Goma huko Kivu kaskazini ambaye amekuwa akiandamana na rais ameiambia RFI Kiswahili tayari ziara hii ya rais Tshisekedi imeanza kuzaa matunda kufuatia hali ya utulivu inayoshuhudiwa hivi sasa kwenye eneo la barabara inayounganisha mji wa Beni na Kaisindi ulioko kwenye mpaka wa DRC na Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.