Pata taarifa kuu
DRC

DRC: Mamlaka ya Kivu Kusini yasitisha shughuli za kampuni tisa za madini

Kampuni tisa za madini, ikiwa ni pamoja na kampuni sita kutoka China, zimesimamishwa kwa muda na mamlaka ya mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wachimbaji katika mgodi ulio wazi mashariki mwa DRC.
Wachimbaji katika mgodi ulio wazi mashariki mwa DRC. AFP - GRIFF TAPPER
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na gavana wa mkoa wa Kivu Kusini, hatua hiyo imechukuliwa ili kurejesha utaratibu katika tasnia ya madini ya dhahabu. Hasa katika eneo la Mwenga, ambalo limekuwa eneo la mvutano kati ya jamii na makampuni hayo ya kigeni ya uchimbaji wa dhahabu.

Kulingana na gavana wa Kivu Kusini, kampuni nyingi za kigeni zinazofanya kazi katika jimbo hilo zinafanya kazi kinyume cha sheria. Hayo yamebainika katika ripoti ya ndani, ameongeza gavana wa mkoa wa Kivu Kusini.

Kampuni zingine zimeanzishwa katika mkoa huo kwa miaka kadhaa. "Wanatua katika mkoa wetu na kibali cha utafiti,"  na mara tu kuanza shughuli yao, wanaendesha shughuli ya uchimbaji wa madini yetu kinyume cha sheria, " amebaini gavana wa Kivu Kusini, Théo Ngwabidje Kasi.

Kulingana na gavana Théo Ngwabidje Kasi, baadhi ya kampuni zimedai kuja kusaidia vyama vya ushirika vya madini. Lakini leo wameanza shughuli ya uzalishaji. Raia pia wanalalamikia juu ya visa vya uchafuzi wa mito.

Gavana anatumai kuwa hitimisho la ripoti hii litawezesha vyombo vya sheria kushughulikia kesi kadhaa na kuokoa sekta hii. Operesheni hii ya ukaguzi itaendeshwa hivi karibuni katika maeneo ya Shabunda, Fizi na Kalehe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.