Pata taarifa kuu
DRC

DRC: Vita vya maneneo vyaibuka kati ya maseneta na Mkaguzi Mkuu wa Fedha

Maseneta nchini Jamhuri ya Kidempkrasia ya Congo wameingia katika vita vya maneneo na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Fedha za serikali baada ya taasis hii kushtumu baadhi ya wabunge kujihusisha na ubadhirifu wa mali ya umma.

Makao makuu ya Bunge, DRC. (Picha ya kumbukumbu)
Makao makuu ya Bunge, DRC. (Picha ya kumbukumbu) Wikimédia
Matangazo ya kibiashara

Tume iliundwa kukabiliana na kiongozi wa  , Jules Alingete. Kulingana na tume hii, atakuwa amekosea kusema kwamba watu wanaotuhumiwa ubadhirifuwa mali ya umaa wameamua kutafuta nafasi katika Bunge ili kutofuatiliwa na vyombo vya sheria baada ya kupata kinga ya ubunge.

Barua inatarajiwa kutumwa kwa rais wa jamhuri ili kuruhusu Bunge la Seneti kumuitisha Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Fedha za serikali awezea kujielea kuhusu matamshi yake.

Suala la Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Fedha za serikali lilitolewa katika mkutano wa Bunge la Seneti mapema wiki hii. Seneta José Makila anasema alikasirishwa na matamshi yake. Amebaini kwamba, Jules Alingete alishindwa kujuwa wajibu wake wa kujizuia kwa kushutumu baadhi ya watu wanaoshukiwa kwa ubadhirifu wa mali ya umma kwa kukimbilia katika Bunge la Seneti ili kuweza kupata kinga ya bunge.

Akishtumiwa kwa kukosea Bunge la Seneti, Jules Alingete anaelezea: "Tunaheshimu sana taasisi za Jamhuri na tunaheshimu wabunge na maseneta wote, na hata maafisa wa serikali. Lakini tunaelezea shida halisi ambayo tunayo katika kushughulikia faili kwa sababu ya kinga. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.