Pata taarifa kuu
DRC

Willy Bakonga, Waziri wa zamani wa Elimu DRC, ahukumiwa kifungo cha miaka 3 jela

Waziri wa zamani wa Elimu wa DRC, Willy Bakonga, ameanza kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya mahakama kumkuta na hatia n akumuhukumu kifungo hicho usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa.

Nchini DRC, Willy Bakonga, Waziri wa zamani wa Elimu, amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela.
Nchini DRC, Willy Bakonga, Waziri wa zamani wa Elimu, amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela. Getty Images/ Spaces Images
Matangazo ya kibiashara

Mwanawe Joël Bakonga amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela. Hii ndio hukumu iliyotolewa na mahakama katika kesi ihusuo ubadhirifu wa mali ya umma.

Waziri wa zamani na katibu wake walikuwa wanashtakiwa kwa kutuma zaidi ya dola 10,000 nje ya nchi.

Aliitishwa siku kumi zilizopita na mahakama kwa tuhuma za ubadhirifu wa kifedha, waziri wa zamani wa elimu ya msingi, sekondari na ufundi hakujibu. Willy Bakonga Wilima alijaribu kutoroka akivuka mto usiku, akiambatana na mwanae, Joël Bakonga, katika jaribio la kusafiri kwa ndege kutoka Brazzaville kwenda Marekani.

Idara za usalama za Congo-Brazzaville zilimkamata na kumrejesha mjini Kinshasa kwa kutumia ndege ya shirika la Air France.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.