Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali: Wanajeshi 15 waangamia katika shambulio katikati mwa Mali

Wanajeshi 15 wa Mali waliuawa katika shambulio la kushtukiza la wanajihadi Alhamisi hii, Agosti 19 katikati mwa nchi, jeshi la Mali limetangaza. Angalau wengine ishirini walijeruhiwa na kupelekwa hospitalini katika mji wa Sévaré.

Askari wa jeshi la Mali katika mazoezi ya kupambana na ugaidi. (Picha ya kumbukumbu).
Askari wa jeshi la Mali katika mazoezi ya kupambana na ugaidi. (Picha ya kumbukumbu). AFP PHOTO / PHILIPPE DESMAZES
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea hasa kati ya miji ya Nokara na Boni katikati mwa Mali. Wanamgambo wa kijihadi wamehusishwa shambulio hilo, ambapo webgi wanajiliza maswalimengi kuhusiana na kuongezeka kwa mashambulizi ya kijihadi nchini Mali.

Shambulizi hilo lililenga msafara wa magari ya jeshi.  Hata hivyo jeshi linadai kwamba liliua wanajihadi wengi, hata kama maiti za wanajihadi hao zilipelekwa na wenzao walipokuwa wakikimbilia msituni.

Kulingana na wachambuzi, wanajihadi watiifu kwa kiongozi wao Amadou Koufa wanataka kwa hali yoyote kudhibiti eneo la kimkakati la Boni, kilomita 60 kutoka mji wa Mondoro na kilomita 90 kutoka mji wa Douenzta. Ili kufanikisha hili, wanajaribu kupinga uwepo wa jeshi ambalo lina kambi iliyoko karibu na kilima huko Boni. Wanajihadi hao wanafanya maisha kuwa magumu kwa raia wanaodaiwa kutoa habari kwa jeshi katika eneo hilo. Katika maeneo mengine, wakulima wanazuiwa kufanya shughuli zao za kilimo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.