Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-SIASA

Wafaransa wawili wakamatwa kwa madai ya kuhatarisha usalama wa taifa Madagascar

Viongozi wa Mashtaka nchini Madagascar wamesema maafisa wa usalama wamezuia jaribio la kumuua rais wa nchi hiyo Andry Rajoelina na watu kadhaa wamekamatwa.

Mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo. (Picha ya kumbukumbu)
Mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo. (Picha ya kumbukumbu) Bernard Gagnon/(CC)/Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa watu waliokamatwa ni raia kadhaa wa Madagascar na raia wa kigeni, wakati huu uchunguzi wa kina ukiendelea kuhusu jaribio hilo.

Aidha, viongozi hao wa mashtaka wanasema kumekuwa na mpango wa kuwauawa viongozi wakuu katika serikjali ya Madagascar akiwemo rais wa nchi hiyo.

Raia wawili wa Ufaransa ni miongoni mwa watu waliokamatwa kwa mujibu wa ripoti za kidiplomasia

Wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya kuadhimisha Uhuru wa nchi hiyo Juni 26, uongozi wa jeshi nchini humo ulisema ulizuia mauaji ya Mkuu wa Majeshi Jenerali Richard Ravalomanana, ambaye ni mshirika wa karibu wa rais Rajoelina. 

Rajoelina, mwenye umri wa miaka 47, aliingia madarakani  kwa mara ya kwanza mwezi Machi mwaka 2009 kutoka kiongozi wa nchi hiyo Marc Ravalomanana kwa usaidizi wa jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.