Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali: Guterres ataka Minusma kuimarishwa na kupewa uwezo zaidi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameliomba Baraza la Usalama kuongeza idadi ya askari wa Minusma, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, kukabiliana na kuongezeka kwa vurugu kutoka kwa makundi ya kijihadi, waraka ambao shirika la habari la REUTERS limepata kopi, umebaini.

Kikosi cha Umoja wa Mataifa Mali, MINUSMA huko Kidal, kaskazini mwa Mali, Septemba 2015 (picha ya kumbukumbu).
Kikosi cha Umoja wa Mataifa Mali, MINUSMA huko Kidal, kaskazini mwa Mali, Septemba 2015 (picha ya kumbukumbu). Photo MINUSMA/Marco Dormino
Matangazo ya kibiashara

Antonio Guterres anaomba, katika ripoti kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya Julai 15 ambayo bado haijatangazwa, kuimarisha tume hiyo kwa zaidi ya wanajeshi 2,000 na maafisa wa polisi na kufikisha jumla ya askari 17,278 wa Minusma, ikiwa ombi hilo litapitishwa itakuwa rekodi ya juu tangu kuanzishwa kwa ujumbe huo mnamo mwaka 2013.

Antonio Guterres ametetea ombi lake kwa kutangaza kwamba kuongezwa kwa askari hao kutasaidia kuwalinda vyema raia katikati mwa Mali dhidi ya ghasia zinazoongezeka za makundi yenye silaha na kuhamasisha mchakato wa amani kaskazini mwa nchi.

Katibu Mkuu wa UN anapendekeza kutuma wanajeshi 1,730 na maafisa wa polisi 339 na kuunda vitengo vitatu vya kuingilia kati haraka, vitakavyojumuisha askari 750 kwa jumla, ikiwa ni pamoja na vitengo vitatu vya helikopta vya watu 260.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.