Pata taarifa kuu
MALI

Karim Keita mtoto wa rais wa zamani wa Mali asakwa

Mahakama nchini Mali imeomba kutolewa kwa waranti ya kimataifa ya kukamatwa kwa Karim Keita mtoto wa rais wa zamani wa Mali anayeshukiwa kuhusika katika mauaji ya mwandishi wa habari wa gazeti la uchunguzi alietoweka miaka mitano iliopita.

Karim Keita  mtoto wa rais wa zamani wa Mali. Julai 11 2018.
Karim Keita mtoto wa rais wa zamani wa Mali. Julai 11 2018. © AFP - Michèle Cattani
Matangazo ya kibiashara

Licha ya vyombo vya habari nchini Mali kuripoti kwamba Karim Keita anafahamu kuhusu kutoweka kwa mwandishi wa habari Birama Toure miaka mitano iliopita, mshukiwa huyo amekuwa akikanusha kutofahamu lolote.

Mkuu wa mahakama kuu jijini Bamako ndiye aliyetaka Polisi ya Kimataifa Interpol kumkamata Karim Keita na kumrejesha nchini Mali kujibu mashtaka yanayo mkabili.

Mwanahabari huyo aliekuwa akifanyakazi katika gazeti la uchunguzi la Sphynx alitoweka katika mazingira tatanishi ambapo vyombo vya habari nchini Mali vinasema kwamba Karim Kéita, mbunge wa zamani, na mtoto wa Rais wa zamani wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta, lazima atakuwa anafahamu kuhusu kutoweka kwake.

Gazeti ambalo mtangazaji Birama Toure alikuwa akifanyia kazi nalo liliripoti kuhusu Karim Keita kuwa anafahamu kuhusu kutoweka kwake, kabla ya kuripoti kuwa huenda aliuawa.

Aliwahi kuhojiwa na vyombo vya sheria wakati akiwa mbunge, lakini kutoka na hadhi yake kama mbunge ilikuwa ngumu kuitishwa mahakamani, lakini sasa sio mbunge na kulingana na vyombo vya sheria nchini Mali kuna taarifa mpya kuhusu kutoweka kwa mwandishi huyo.

Kwa taarifa tulizozipata ni kwamba Karim Keita anaishi ugenini katika nchi jirani na Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.