Pata taarifa kuu
RWANDA-DIPLOMASIA

Marais wa Rwanda Paul Kagame na Felix Tshisekedi wa DRC wamekutana Rubavu Ijumaa hii

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ikulu ya rais jijini Kinshasa, inasema viongozi hawa wawili Paul Kagame wa Rwanda naye rais Felix Tshisekedi wanakutana hivi leo kujadili uwezekano wa nchi ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC kuingizwa katika jumuia ya nchi za Afrika mashariki EAC lakini pia wata Jiji la Rubavu kutathmini uharibifu uliosababishwa na matetemeko ya ardhi yaliyofuata mlipuko wa volkano wa Nyiragongo hivi karibuni.

Marais Paul Kagame wa Rwanda na rais Felix Tshisekedi wa DRC wakiteta kuhusu mahusiano ya kidiplomasia kati ya Nchi zao, Marchi 2021
Marais Paul Kagame wa Rwanda na rais Felix Tshisekedi wa DRC wakiteta kuhusu mahusiano ya kidiplomasia kati ya Nchi zao, Marchi 2021 © Ikulu ya Kinshasa DRC
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya kiusalama kutoka mjini Gisenyi unaopakana na jiji la Goma upande wa DRC vimebainisha kuwa punde baada ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na volcano, viongozi hawa wawili watafanya mazungumzo ya pande mbili ambayo yatajikita juu ya namna ya kuboresha mahusiano ya kidiplomasia baina ya mataifa hayo mawili jirani, suala la DRC kujiunga na jumuia ya afrika mashariki lakini pia usalama wa mashariki ya DRC.

Katika hatua nyingine rais Paul Kagame atafanya ziara fupi ya kikazi katika mji wa Goma mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini upande wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambapo atapokelewa na mwenyeji wake Rais Tshisekedi siku ya jumamosi.

Wakuu hao wawili watatembelea maeneo yaliyoharibiwa na mlipuko wa mlima wa volkano wa Nyiragongo upande wa mpaka wa DRC, maeneo ya kibati, na kilimanyoka kabla ya kukutana katika dhifa maalum, iliyoandaliwa katika hoteli ya kifahari ya serana mjini Goma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.