Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-UCHAGUZI 2021

Wananchi wa Ethiopia wanapiga kura katika uchaguzi ulioahirishwa mara mbili

Wananchi wa Ethiopia wanapiga kura, kwenye uchaguzi unaofuatiliwa kwa karibu duniani, wakati huu nchi hiyo inapokabiliwa na ukame hasa kwenye jimbo lenye mzozo la Tigray.

Upiigaji kura nchini Ethiopia Juni 21 2021
Upiigaji kura nchini Ethiopia Juni 21 2021 AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu unafanyika, baada ya kuahirishwa mara mbili, na mtihani kwa Waziri Mkuu Abiy Ahmed ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2018.

Wapiga kura walianza kuwasili katika vituo vya kupigia kura mapema alfajiri huku upigaji kura ukianza saa kumi na mbili na dakika 10 saa za Afrika Mashariki.

Wapiga kura Milioni 38 wanawachagia wabunge wa kitaifa na wale wa majimbo, na baadaye wabunge watamchagua Waziri Mkuu, lakini uchaguzi huo haufanyiki katika jimbo la Tigray, huku maeneo mengine ambayo uchaguzi huu haufanyiki kwa sababu za kiusalama, ukipangwa kufanyika tarehe sita mwezi Septemba.

Yordanos Berhanu, aliyekuwa miongoni mwa wapiga kura wa kwanza ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa, anaamini kuwa uchaguzi huu, utawasha mwanga wa demokrasia nchini Ethiopia.

Wachambuzi wa siasa tayari wanaona kuwa chama tawala, Prosperity Party cha Waziri Mkuu Ahmed ambacho kinawagombea wengi katika uchaguzi huu, kipo katika nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo na kuunda serikali ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.