Pata taarifa kuu
ETHIOPIA UN

Ethiopia: Addis Ababa yatupilia mbali onyo la UN kuhusu njaa huko Tigray

Njaa katika eneo lenye mgogoro la Tigray inaelekea kuenea kwa majimbo mengine ya Ethiopia, Katibu Mkuu Kiongozi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu alionya Jumanne katika mkutano wa Baraza la Usalama lililofanyika faraghani. Njaa sasa inatishia karibu Waethiopia milioni 2.5, kulingana na Mark Lowcock. Balozi wa Ethiopia kwenye Umja wa Mataifa UN ameshutumu na kutupilia mbali tahadhari hiyo.

Mwanamke aliebebe mwanae wakisubiri kupewa chakula
Mwanamke aliebebe mwanae wakisubiri kupewa chakula REUTERS - BAZ RATNER
Matangazo ya kibiashara

Kwa majuma kadhaa Mark Lowcock amekuwa akilionya Baraza la Usalama na umma kwa jumla: watu 350,000 tayari wamezama kwenye njaa huko Tigray. Milioni mbili zaidi, huko Tigray, Afar na Amhara, sasa pia inaaminika kuwa chini ya tishio. "Njaa iliyosababishwa na watu," Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa Barbara Woodward alilaumu mbele ya Baraza lililoshindwa kuungana kutoa taarifa ya pamoja.

Miezi saba baada ya operesheni ya haraka ilioanzishwa na waziri mkuu, tuko mbali kutoka kwa operesheni ya haraka iliyoahidiwa na Abiy Ahmed wakati alipotuma jeshi la shirikisho Tigray kuwashinda waasi. Wengi katika baraza wana wasiwasi juu ya kuendelea kwa mapigano na karibu matumizi ya ubakaji.

Balozi wa Ethiopia katika UN, Taye Atske Selassie Amde, alilalamika mwishoni mwa mkutano kwamba Baraza la Usalama linajadili hali ya Tigray, ambayo sio kwenye ajenda yake, na ambayo kulingana na Addis Ababa, hiy ni mada ya sera ya ndani zaidi. Anakanusha pia takwimu za utapiamlo zilizotolewa na mashirika ya Umoja wa Mataifa. "Hatukubaliani kabisa na tathmini hii" ya UN juu ya njaa, aliwaambia waandishi wa habari, akiamini kwamba data iliyokusanywa na UN pamja na NGOs haikuwa ya wazi.

Mkutano wa mwisho wa Baraza la Usalama kuhusu Tigray ulifanyika Aprili 22. Halafu ilipitisha tamko la kwanza la pamoja la kushutumu unyanyasaji katika mkoa huu wa kaskazini mwa Ethiopia.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2019, mnamo Novemba alituma jeshi la shirikisho kwa Tigray kupigana na TPLF (Mbele ya Ukombozi wa Watu wa Tigray), wakati huo ikiwa madarakani kijijini na ambayo iliipa changamoto serikali kuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.