Pata taarifa kuu
CHAD

Mapigano nchini Chad: Kundi la waasi la FACT laondoka Kanem

Mapigano yanaendelea katika mkoa wa Kanem ambapo mapigano yalizuka Jumamosi alasiri, Aprili 17. Vikosi vya jeshi vya Chad vimekuwa vikikabiliana kwa wiki moja na kundi la waasi la FACT, Front for Alternation and Concord in Chad, baada ya kupitia kaskazini mwa nchi kutoka ngome yake kuu nchini Libya wiki moja iliyopita.

Katika picha hii iliyotolewa na jeshi la Chad Aprili 18, waasi wanaoshukiwa kuwa wa kundi la FACTwamekamatwa kufuatia makabilaino na wanajeshi huko Nyze, Kanem, Aprili 17.
Katika picha hii iliyotolewa na jeshi la Chad Aprili 18, waasi wanaoshukiwa kuwa wa kundi la FACTwamekamatwa kufuatia makabilaino na wanajeshi huko Nyze, Kanem, Aprili 17. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano na RFI, kiongozi wa kundia la FACT Mahamat Mahadi Ali amekiri kwamba wapiganaji wake wameamua kuondoka katika mji wa Kanem katika kujianda upya jinsi ya kukabiliana na vikosi vya serikali.

Kulingana na duru za kuaminika, mapigano yaliendelea Jumapili na hadi asubuhi ya Jumatatu, Aprili 19. Mapigano ambayo inasemekana yalitokea karibu na mji wa Nokou, kilomita 50 kutoka mji wa Mao, mji mkuu wa mkoa wa Kanem. Mkoa wa Kanem unapatikana katikati mwa magharibi mwa Chad na unaendelea kwenye mpaka na Niger.

Kiongozi wa FACT amebaini kwamba idadi kubwa ya wapiganaji imetumwa kaskazini mwa nchi, bila kutoa maelezo zaidi. Amesema "wanafikiria juu ya hatua watakazo chukuwa katika siku za hivi karibuni".

Ufaransa yaonyooshewa kidole cha lawama

Mahamat Mahadi Ali ameishtumu Ufaransa kumsaidia Idriss Deby katika mapigano hayo hasa kwa kumpa taarifa za kijasusi baada ya ndege za Ufaransa kuendelea kufanya operesheni za kijasusi karibu na maeneo wanayoshikilia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.