Pata taarifa kuu
CHAD

Jeshi la Chad ladai kuwatimua waasi karibu na mji mkuu N'Djamena

Jeshi la Chad limesema limezuia shambulio la waasi na kuwarejesha nyuma baada ya kujaribu kuelekea mji mkuu N'Djamena, wakati nchi hiyo inasubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa urais wa Aprili 11.

Watu wanapita katibu na gari la jeshi la Chad karibu na ikulu ya rais, wakati wapiganaji kutoka chama cha waasi cha Front for Alternation and Concord in Chad (FACT) walionekana wakielekea mji mkuu kulingana na Marekani, huko N'djamena, Chad Aprili 19, 2021.
Watu wanapita katibu na gari la jeshi la Chad karibu na ikulu ya rais, wakati wapiganaji kutoka chama cha waasi cha Front for Alternation and Concord in Chad (FACT) walionekana wakielekea mji mkuu kulingana na Marekani, huko N'djamena, Chad Aprili 19, 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Kundi cha waasi lenye makao yake nchini Libya, Front for Alternation and Concord in Chad (FACT), ambalo limekuwa likisonga kuelekea kusini mwa nchi baada ya kushambulia kituo cha vikosi mpakani siku ya uchaguzi wa urais, wakitaka kumalizika kwa utawala waIdriss Déby, ambaye yuko madarakani kwa muda wa miaka 30.

Msemaji wa jeshi Azem Bermendao Agouna ameliambia shirika la habari la REUTERS kwamba vikosi vya Chad vimewaua waasi zaidi ya 300 na kukamata 150 katika vita ambavyo vilifanyika Jumamosi katika mkoa wa Kanem, karibu kilomita 300 kutoka mji wa N'Djamena. Wanajeshi watano waliuawa na wengine 36 walijeruhiwa, ameongeza.

Deby ashinda uchaguzi kwa 84%

Idriss Déby, mmoja wa viongozi waliodumu madarakani kwa muda mrefu barani Afrika, anaonekana yuko tayari kupata muhula wa sita wa uongozi wa nchi.

Hata hivyo upinzani umesema kuwa hakuna uchaguzi uliofanyika nchini Chad. Viongozi wa upinzani walitoa wito kwa wafuasi wao kususia uchaguzi wa wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.