Pata taarifa kuu
DRC

Mkuu wa MONUSCO atiwa wasiwasi na wito wa vurugu mashariki mwa DRC

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Mkuu wa tume ya umoja huo, MONUSCO, Bintou Keita, ameelezea wasiwasi wake kufuta kuongezeka kwa wito wa vurugu na chuki katika maeneo ya Beni, Butembo na Lubero, dhidi ya mashirika ya kutoa misaada na mashirika ya kimataifa, hasa MONUSCO.

Wanajeshi wa Monusco wapiga doria karibu na mahali ambapo shambulio lilitokea Februari 22, 2021.
Wanajeshi wa Monusco wapiga doria karibu na mahali ambapo shambulio lilitokea Februari 22, 2021. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Katika siku za hivi karibuni, mashirika kadhaa ya kiraia katika mkoa wa Kivu Kaskazini yaliitisha maandamano, hasa dhidi ya MONUSCO, ambayo wanaituhumu kutofanya vya kutosha dhidi ya makundi yenye silaha katika eneo la Beni.

"Umoja wa Mataifa umeshikamana na uhuru wa kujieleza, maoni na maandamano ya amani na unakumbusha kwamba maandamano ya amani yanaweza kutumika kwa njia halali bila wito wowote wa vurugu dhidi ya watu binafsi au mashirika," alisema msemaji wa tume ya Umoja wa Mataifa, Mathias Gillman, Jumatano wiki hii wakati wa mkutano wa kila wiki wa Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari.

MONUSCO inasema "inaelewea na inahuzunishwa na hali inayowakabili raia kwa kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya raia, uhalifu unaotekelezwa hasa na kundi la waasi wa Uganda wa ADF".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.