Pata taarifa kuu
MONUSCO

DRC: Jean-Pierre Lacroix akutana na wajumbe kutoka FCC na upinzani

Mgogoro wa kisiasa nchini DRC umejadiliwa wakati wa mazungumzo kati ya Jean-Pierre Lacroix na viongozi wa kisiasa nchini DRC.

Ndege ya kivita ya jeshi la MONUSCO
Ndege ya kivita ya jeshi la MONUSCO RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani Jean-Pierre Lacroix aliwasili Kinshasa Jumapili jioni.

Wengi wa washiriki katika mkutano huo wamebaini kwamba mgogoro wa kisiasa upo.

Kwa upande wa Nehemia Mwilanya, mratibu wa muungano wa FCC, amebaini kwamba 'kwa kweli kuna mgogoro wa kisiasa. mgogoro huu unatokana na kuvunjika kwa muungano wa kisiasa kati ya FCC ya Joseph Kabila na CACH ya Félix-Antoine Tshisekedi.

Nehemia Mwilanya amesema amezungumza na Jean-Pierre Lacroix juu ya kuvunjika kwa mkataba wa imani katika muungano tawala.

Jean-Pierre Lacroix pia alikuwa na mazungumzo na viongozi wawili wa Lamuka, Adolphe Muzito na Martin Fayulu.

Kulingana na Adolphe Muzito, mgogoro huu ni moja ya uhalali ambao utalazimika kutatuliwa kwa kuzingatia uchaguzi wa 2023.

Jumanne hii, Jean-Pierre Lacroix anatarajia kupokelewa kwa mazungumzo na rais wa Félix-Antoine Tshisekedi kabla ya kusafiri kwenda katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri, eneo ambalo makundi yenye silaha bado yanaendelea na hujuma zao na ambapo ukosefu wa usalama dhidi ya raia unaendelea kuripotiwa.

Mnano Desemba 20 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litalazimika kuamua juu ya hatma ya mamlaka ya MONUSCO nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.