Pata taarifa kuu
DRC-MONUSCO

DRC: Umoja wa Mataifa yaongeza muda wa MONUSCO

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa mwaka mmoja kwa tume yake ya kulinda amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, kuendelea na shughuli zake nchini humo.

Butembo, Kivu Kaskazini, DR Congo. Mnamo tarehe 22 Februari 2018, askari wa MONUSCO waliwatimua mara moja wapiganaji 1000 wa kundi la waasi la Mai Mai 100 katika kijiji cha Vuhovi, mashariki mwa Butembo.
Butembo, Kivu Kaskazini, DR Congo. Mnamo tarehe 22 Februari 2018, askari wa MONUSCO waliwatimua mara moja wapiganaji 1000 wa kundi la waasi la Mai Mai 100 katika kijiji cha Vuhovi, mashariki mwa Butembo. ©MONUSCO
Matangazo ya kibiashara

Azimio lililoandaliwa na Ufaransa limepitishwa na wanachama 14 kati ya 15 wa Baraza la Usalama la Umoja la Mataifa, huku Urusi ikikijizuia kupiga kura.

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO itaendelea na shughuli zake za kulinda amani hadi Desemba 20, 2021", ikiwa na askari na maafisa wa polisi karibu 16,300.

Azimio hilo limeitaka sekretarieti ya Umoja aw Mataifa "kuzingatia zaidi namna ya kupunguza idadi ya askari wa kikosi hicho na kupunguza maeneo ya operesheni zake kulingana na jinsi hali ya usalama inavyoendelea katika nchini humo, hasa katika mikoa ambayo ambapo hakuripotiwi tena vitisho kutoka makundi yenye silaha".

Baraza la Usalama la Umoja aw Mataifa "linaidhinisha" mpango wa pamoja wa UN-DRC uliowasilishwa mnamo mwezi Oktoba "kujiondoa hatua kwa hatua kwa MONUSCO nchini DRC " kwa lengo la kukabidhi majukumu yanayoshikiliwa na walinda amani kwa vikosi vya DRC, lilisomeka azimio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.