Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Mazungumzo kati ya Misri, Ethiopia na Sudan yaambulia patupu

Mazungumzo ya hivi punde kati ya Misri, Ethiopia na Sudan kuhusu matumizi ya maji ya mto Nile kutumiwa kwenye bwawa kubwa la kuzalisha umeme nchini Ethiopia, yamemalizika bila ya makubaliano yoyote.

Bwawa la Renaissance lililojengwa nchini Ethiopia katika mkoa wa Benishangul Gumuz, kwenye Mto Nile, Machi 2015.
Bwawa la Renaissance lililojengwa nchini Ethiopia katika mkoa wa Benishangul Gumuz, kwenye Mto Nile, Machi 2015. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Wawakilishi wa nchi hizo tatu, walikutana kwa mazungumzo ya kutafuta mwafaka kuhusu mvutano huo jijini Kinshasa nchini DRC, yalimalizika siku ya Jumanne bila ya maelewano.

Wizara ya Mambo ya nje ya Misri imesema, mazungumezo hayo yalivunjika baada ya Ethiopia kukataa pendekezo la Sudan, kutaka wasuluhishi wa kimataifa kuhusishwa katika mazungumzo hayo.

Imebainika kuwa Ethiopia haitaki Marekani, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, kuhusishwa katika mazungumzo hayo, msimamo ambao Sudan na Misri zinasema, Ethiopia haioneshi utashi wa kisiasa kuhusu mvutano huo.

Ethiopia kwa upande wake haijasema chochote kuhusu kuvunjika kwa mazungumzo hayo, lakini imekuwa ikisisitiza kuwa mradi wake unalenga kuimarisha uchumi wake kuzalisha umeme kwa ajili ya watu wake kupitia bwawa hilo kubwa la kuzalisha umeme barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.