Pata taarifa kuu
CAR

CAR: Wataalam wa UN watiwa wasiwasi kuhusu dhulma za mamluki kutoka Urusi

Kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake  juu ya ripoti za "ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu", uhalifu unaotekelezwa na mamluki kutoka Urusi wanaosaidia jeshi la Afrika ya Kati katika vita vyake dhidi ya waasi, kulingana na taarifa iliyotolewa Jumatano (Machi 31) mjini Geneva.

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati inayooshewa kidole cha lawama kwa kufumbia macho uhalifu unaotekelezwa na mamluki kutoka Urusi.
Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati inayooshewa kidole cha lawama kwa kufumbia macho uhalifu unaotekelezwa na mamluki kutoka Urusi. © AFP/FLORENT VERGNES
Matangazo ya kibiashara

"Wataalam wamepokea, na wanaendelea kupokea, ripoti za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria ya kimataifa ya kibinadamu, uhalifu unaotekelezwa na mamluki wanasaidia vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA) na, wakati mwingine, na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, ”Wamesema wajumbe wa kundi hili la wataalam wa Umoja wa Mataifa.

Ni uchunguzi unaotia hatiani Umoja wa Mataifa, Baraza lake la Usalama na operesheni zake za kulinda amani.

Katika taarifa iliyochapishwa Jumatano, kundi hili la wataalam wanaofanya kazi kuhusu kutumiwa kwa mamluki, linashutumu Tume ya Umoja wa Mataifa inayosimamia amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) kwa kushirikiana na wanamgambo wa kampuni ya kibinafsi ya usalama kutoka Urusi, Wagner, na kuwa imeshahidia unyanyasaji uliofanywa mamluki hao.

Kundi hili linalofanya kazi ambalo linaundwa na wataalam wa kujitegemea, wanachunguza chini ya taratibu maalum za Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, kwa hivyo inathibitisha habari iliyochapishwa na Ukombozi mnamo Februari 1.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.