Jamhuri ya Afrika ya Kati yaiweka kwenye himaya yake ngome ya waasi ya Bossangoa
Jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati, likisaidiwa na washirika wake Urusi na Rwanda, wanadhibiti tena ngome ya waasi ya Bossangoa tangu Jumatano wiki hii, serikali imesema katika taarifa.
Imechapishwa:
Mlipuko wa machafuko yanayohusishwa na uchaguzi wa urais uliofanyika Desemba 27 umesababisha zaidi ya watu 200,000 kuyatoroka makaazi yao, hali ambayo imeendelea kusababisha bei za bidhaa mahitajio kupanda kutokana na kukosekana hali ndogo ya usalama kwa magari yanayosafirisha chakula katika maeneo mbalimbali nchini humo.
Waasi wanaosadikiwa kushirikiana na rais wa zamani François Bozizé waliudhibiti mji wa Bossangoa, mji alikozaliwa unaopatikana kilomita 260 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Bangui, na miji mingine kadhaa baada ya Mahakama ya Katiba kutoidhinisha kuwania kwake mnamo mwezi Desemba.
Nchi hiyo, yenye utajiri wa dhahabu na almasi, na yenye wakaazi karibu milioni 5, imeshindwa kupata utulivu tangu kuzuka kwa uasi wa mwaka 2013.