Pata taarifa kuu

UN: Viwango vya utapiamlo kwa watoto vyaongezeka CAR

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yameonya juu ya machafuko na ukosefu wa usalama vinazokwamisha shughuli zao nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Angalau watoto 24,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano kwa sasa wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa utapiamlo sugu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kulingana na UNICEF na shirila la Mpango wa Chakula duniani (WFP).
Angalau watoto 24,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano kwa sasa wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa utapiamlo sugu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kulingana na UNICEF na shirila la Mpango wa Chakula duniani (WFP). © Charlotte Cosset/RFI
Matangazo ya kibiashara

Shirika·la·Umoja·wa·Mataifa·la·kuhudumia·watoto·UNICEF·na·Shirika·la·mpango·wa·chakula·duniani·WFP·wanasema·wana·wasiwasi·juu·ya·watoto·walio·katika·hatari·ya·kupata·ugonjwa·wa·utapiamlo·sugu.

Angalau·watoto·24,000·walio·na·umri·wa·chini·ya·miaka·mitano·kwa·sasa·wako·katika·hatari·ya·kupata·ugonjwa·wa·utapiamlo·sugu·nchini·Jamhuri·ya·Afrika·ya·Kati,·kulingana·na·UNICEF·na·shirila·la·Mpango·wa·Chakula·duniani·(WFP).·

Mashirika·haya·mawili·ya·Umoja·wa·Mataifa·kwa·miaka·mingi·yanaendesha·shughuli·zao·katika·nchi·hii·inayochukuliwa·kama·moja·ya·nchi·maskini·zaidi·duniani.·Sio·mara·ya·kwanza·kukabiliwa·na·aina·hii·ya·matatizo,·lakini·mwaka·huu·visa·vya·utapiamlo·vimeongezeka·kwa·25%·ikilinganishwa·na·mwaka·2020.·Sababu·ni·janga·la·Covid-19,·lakini·pia·vurugu·ambazo·uingiliaji·wa·haraka·ili·kuepuka·hali·mbaya·zaidi·umekuwa·ukichelewa.

"Bila·kupata·huduma·ya·haraka·wanayohitaji,·watoto·wenye·utapiamlo·wako·katika·hatari·ya·kifo"·,·Fran·Equiza,·mwakilishi·wa·UNICEF·​​nchini·Jamhuri·ya·Afrika·ya·Kati·amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.