Pata taarifa kuu
MISRI

Shughuli zaendelea kwenye Mfereji wa Suez , zaidi ya meli 100 zavuka

Zaidi ya meli 100 zimevuka Mfereji wa Suez kwa pande zote mbili tangu meli kubwa ya kontena ambayo ilikuwa imekwamisha urambazaji kwa karibu wiki moja kurejeshwa majini, Televisheni ya serikali ya Misri imeripoti leo Jumanne.

Karibu meli 113 zilikuwa zimevuka kupitia mfereji huo saa 12 asubuhi, kulingana na mipango iliyotangazwa hapo awali na Mamlaka ya Mfereji wa Suez (ACS)..
Karibu meli 113 zilikuwa zimevuka kupitia mfereji huo saa 12 asubuhi, kulingana na mipango iliyotangazwa hapo awali na Mamlaka ya Mfereji wa Suez (ACS).. AP
Matangazo ya kibiashara

Karibu meli 113 zilikuwa zimevuka kupitia mfereji huo saa 12 asubuhi, kulingana na mipango iliyotangazwa hapo awali na Mamlaka ya Mfereji wa Suez (ACS).

Osama Rabie, mwenyekiti wa CSA, ameelezea kwamba meli zingine 140 pia zinatarajiwa kuvuka mfereji wa Suez Jumanne: meli 95 ifikapo saa moja usiku, kwa saa za Misri, na 45 zaidi kabla ya saa sita usiku.

Amesisitiza pia kwamba itachukua siku tatu hadi nne kwa kuokoa muda ulipotea ambao uliosababishwa na tukio hilo.

Shughuli zilianza tena kwenye Mfereji wa Suez Jumatatu jioni baada ya Meli inayojulikana kwa jina la Ever Given, meli yenye urefu wa mita 400 ambayo ilikwama Jumanne ya wiki iliyopita katikati ya sehemu ya mfereji, kurejeshwa majini siku hiyo.

Kushindwa kuinasua meli hiyo kulisababisha msongamano mkubwa wa meli baharini ambapo meli zaidi ya 400 zilisubiri kuweza kuvuka Mfereji wa Suez.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.