Pata taarifa kuu
UN-AL-QAEDA

Video: Kiongozi wa Al-Qaeda katika Rasi ya Arabia bado ana nguvu

Kiongozi wa al-Qaeda katika Rasi ya Arabia (Aqpa) anaonekana bado yuko hai na ana nguvu, kulingana na video ya hivi karibuni inayomuonyesha, kinyume na ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo ilisema yuko kizuizini, shirika la utafiti juu ya makundi yenye msimamo mkali, SITE Intelligence Group, na wakuu wawili wa makabila wamesema.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Mmoja wa viongozi wa dunia wanaopambana na kundi la Al Qaeda.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Mmoja wa viongozi wa dunia wanaopambana na kundi la Al Qaeda. Thibault Camus/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Khalid Batarfi, anayejulikana kama Abu Miqdad el-Kindi na kiongozi kwa karibu mwaka mmoja wa tawi hili la Al-Qaeda anayechukuliwa kuwa hatari sana, alionekana kwenye video hiyo iliyorushwa Jumatano wiki hii, akizungumzia kuhusu shambulio la wafuasi wa Donald Trump huko Capitol ambalo lilifanyika mwezi uliopita.

 

Katika video hii ya dakika ishirini, Batarfi anasema, akimaanisha Marekani, kwamba shambulio dhidi ya makao makuu ya Bunge la Congress lililotekelezwa na wafuasi wa rais wa zamani wa Marekani ni "maumivu madogo ya kile kinachowasubiri, Mungu akipenda".

 

Ripoti iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita inadai kwamba Khalid Batarfi "alikamatwa mnamo mwezi Oktoba wakati wa operesheni huko Gheida (mkoa wa Mahra), operesheni ambayo pia ilisababisha kifo cha naibu wake, Saad Atef el-Aoulaqi".

 

Hati hiyo haikufafanua ni nani aliyemkamata Batarfi , na ikoje tangu wakati huo.

 

Lakini kulingana na viongozi wawili wa makabila katika eneo la Al-Bayda katikati mwa Yemen ambako Al-Qaeda inaendesha vitendo vyake viovu, kuna uwezekano mkubwa kwamba mtu aliyekamatwa kulingana na Umoja wa Mataifa ni mwanachama mwingine wa kundi hilo la kijihadi.

 

Al-Qaeda katika Peninsula ya Arabia ilidai kumteua Batarfi, ambaye anaaminika kuwa na umri wa miaka arobaini, kama kiongozi wake mwezi Februari 2020 baada ya kifo cha mtangulizi wake Qassem al-Rimi kufuatia shambulio la angani la Marekani huko Yemen.

 

- Tawi hatari zaidi -

 

Batarfi, anachukuliwa kama gaidi wa kimataifa na Marekani tangu mwaka 2018, amejitokeza kwenye video mara kadhaa, kulingana na shirika la utafiti juu ya makundi yenye msimamo mkali, SITE Intelligence Group

 

Kundi la Aqpa liloundwa mnamo mwaka 2009, linachukuliwa na Marekani kama tawi hatari zaidi la mtandao wa kijihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.