Pata taarifa kuu
MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Mali yasubiri kuondolewa vikwazo vya ECOWAS

Baada ya mazungumzo ya siku kadhaa, Waziri Mkuu mpya wa Mpito ameteuliwa tangu jana Jumapili septemba 27. Moctar Ouane, mwanadiplomasia na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje, ndiye ameteuliwa kushikilia wadhifa.

Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Mali, Bamako.
Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Mali, Bamako. GettyImages
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuapishwa kwa rais na makamu wa rais, tayari kizuizi kiliokuepo kimeondolewa, lakini Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi bado haijaondoa vikwazo vyake dhidi ya nchi hiyo viliviwekwa baada ya kundi la maafisa wa jeshi kufanya mapinduzi dhidi ya utawala wa Ibrahim Boubacar Keita.

Kwa mtazamo wa wengi, vikwazo vya ECOWAS dhidi ya Mali vingelikuwa tayari kuondolewa. Lakini saa 24 baada ya uteuzi wa Waziri Mkuu, bado Mali inakabiliwa na vikwazo hivyo. Bado kuna matumaini katika saa kadhaa zijazo kwamba huenda vikwazo hivyo vikaondolewa.

Wakati wa ziara yake ya mwisho jijini Bamako, mpatanishi wa ECOWAS, Goodluck Jonathan alithibitisha kwamba "jumuiya hiyo bado haikupokea toleo la mwisho la hati ya mpito", ikimaanisha waraka hati ambayo inathibitisha kipindi cha mpito cha miezi 18.

Maelezo zaidi yasubiriwa

Katika hati hii, ECOWAS inasubiri kupata ufafanuzi zaidi. Kwa sasa, katika toleo la hati ambayo inazunguka, inabaini kwamba makamu wa rais, ambaye ni kiongozi wa mapinduzi ya Agosti 18, anaweza kuchukua nafasi ya rais wa mpito ikiwa atashindwa kutimiza wajibu Hata hivyo ECOWAS, haikubaliani na hoja hiyo. Kuna ulazimakipengele hicho kiondolewa kwenye hati hiyo.

Matarajio mengine ya raai aw Mali ni serikali ya mpito. Kwa wakati wowote serikali hiyo inaweza kutangazwa. M5, vuguvgu hili lililoanzishwa Juni 5 ambalo linadai kuwa lilichangia hasa kwa kuangusha utawala wa IBK, linajadili kupata nyadhifa kwenye srikali mpya.

Vuguvugu hili la M5 halikuhusishwa katika uteuzi wa rais au wa makamu wa rais wa Mpito. Na kwenye wadhifa wa Waziri Mkuu, kundi hili liliwasilisha fali 14 za wagombea kwenye nafasi hiyo. Wagombea kumi na wanne walijikuta wameangushwa na Moctar Ouane.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.