Pata taarifa kuu
MALI-SIASA-USALAMA

Umati wa watu wamiminika mitaani Bamako kuunga mkono kundi la wabajeshi waliofanya mapinduzi

Mamia ya watu wameandamana jijini Bamako nchini Mali, kuonesha uungwaji mkono kwa viongozi wa jeshi waliomwondoa madarakani rais wa zamani Ibrahim Boubakar Keita mwezi uliopita.

Watu waliokusanyika karibu na eneo la Uhuru huko Bamako, Agosti 19, 2020 (picha ya kumbukumbu).
Watu waliokusanyika karibu na eneo la Uhuru huko Bamako, Agosti 19, 2020 (picha ya kumbukumbu). AP Photo/Atouna Sissoko
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya viongozi wa nchi za Afrika Magharibi kuwataka wanajeshi hao kuhakikisha kuwa wanakabidhi madaraka kwa raia, baada ya mwaka mmoja baada ya mazungumzo ya siku ya Jumatatu.

Mapema wiki hii Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ilitangaza kwamba inaendelea na vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Bamako na dhidi ya Kamati ya Kitaifa ya Wokovu wa wananchi (CNSP), wanajeshi waliochukua madaraka baada ya kumpindua rais Ibrahim Boubacar Keïta.

Uamuzi huu ulichukuliwa katika mkutano wa viongozi wa nchi hizo waliokutana Jumatatu hii Septemba 7 huko Niamey, mji mkuu wa Niger. Mkutano ambao uliangazia hali inayoendelea nchini Mali, baada ya jeshi kupindua aliyechaguliwa Ibrahim Boubacar Keita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.