Pata taarifa kuu
MALI-SIASA-USALAMA

Mali: Jeshi lafanya mazungumzo na washirika wa IBK, upinzani wasubiri

Viongozi wa kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Mali, ikiwa ni pamoja na Makamu wa rais Kanali Malick Diaw, na msemaji wa kundi hilo Meja-Kanali Ismaël Wagué wameanza mikutano kadhaa na wadau mbalimbali nchini humo tangu Alhamisi wiki hii.

Kanali Malick Diaw, makamu wa rais wa CNSP, anawasili katika makao makuu ya wizara ya ulinzi ya Mali kwa mkutano na vyama vya walio wengi Agosti 20, 2020.
Kanali Malick Diaw, makamu wa rais wa CNSP, anawasili katika makao makuu ya wizara ya ulinzi ya Mali kwa mkutano na vyama vya walio wengi Agosti 20, 2020. MALIK KONATE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wamekutana na vyama vya siasa vya walio wengi. Mkutano huu wa kwanza ulikuwa kwanza kufahamiana, lakini mmoja miongoni mwa walioshiriki mkutano huo alipewa nafasi ya kutoa maoni yake kuhusu mustakabali wa nchi hiyo.

Upinzani kwa upande wake unasubiri kukutana na kundi hilo la wanajeshi.

Mkutano huo ulifanyika katika Wizara ya Ulinzi ya Mali, kama alivyobaini mwandishi wetu huko Bamako, Serge Daniel.

Waakilishi wa vyama vya walio wengi, washirika wa karibu wa rais IBK wamefurahishwa na mazungumzo na mazungumzo hayo. "mazungumzo au niseme tu mkutano umekwenda vizuri!, " amesema Djibril Tall, kiongozi wa chama cha PDES, kinachomuunga mkono rais IBK, ambaye amesema hana hofu kuwa jeshi linaweza kusalia madarakani kwa muda mrefu.

Hata hivyo baadhi ya vyama vya walio wengi, vimelaani jaribio hilo la mapinduzi.

"Watu wanalaani mapinduzi ya kijeshi. Wanataka rais wa Jamhuri aachiliwe huru, angalau raia wapewe nafasi ya kumuona, " amesema Djiguiba Kéita, anayejulikana kwa jina maarufu la PPR, wa Chama cha Parena.

Milango ya mazungumzo na kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi haijafungwa, lazima tusonge mbele, amebaini Blaise Sangaré, kiongozi mwengine wa vyama vya walio wengi: "Kuna mgogoro ndani ya mgogoro, tayari kulikuwa na mgogoro kubwa wa kijamii na kisiasa, kwa hiyo tunatakiwa kwanza kutafuta suluhu mgogoro wa kisiasa."

Hivi karibuni kundi hilo la wanajeshi litakutana na wadaui wengine nchini Mali, ikiwa ni pamoja na upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.