Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-USALAMA-SIASA

Visa vya ukandamizaji vyaendelea kuongezeka Zimbabwe

Hali ya mvutano inaendelea kuongezeka nchini Zimbabwe wakati yakikaribia maandamano ya upinzani dhidi ya ufisadi katika serikali, yaliyopangwa kufanyika Ijumaa (Julai 31).

Katibu mkuu wa chama cha upinzani cha MDC-Alliance anashikiliwa na polisi katika makao makuu ya chama huko Harare mnamo Juni 5, 2020.
Katibu mkuu wa chama cha upinzani cha MDC-Alliance anashikiliwa na polisi katika makao makuu ya chama huko Harare mnamo Juni 5, 2020. Jekesai NJIKIZANA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu, polisi iliendesha operesheni ya kuwasaka wanaharakati wa upinzani.

Katika taarifa, vikosi vya usalama viliomba kupewa taarifa kuhusu eneo wanakopatikana wanasiasa kumi na nne wa upinzani.

Mwanaharakati Peter Mutasa, mbunge wa upinzani Job Sikhala na viongozi wa mashirika ya kiraia, ni miongoni mwa wanaharakati hao wanaotafutwa na polisi.

Wito huo unakuja siku chache baada ya kukamatwa, wiki iliyopita, mwandishi wa habari Hopewell Chinofu na kiongozi wa chama kidogo cha siasa, Jacob Ngarivhume, wote wawili waliitisha maandamano Julai 31.

Watu hao wawili bado wanazuiliwa kwa tuhuma za kuchochea ghasia. Mabalozi kadhaa, ikiwa ni pamoja na balozi wa Marekani, wameelezea wasiwasi wao kuhusu ukandamizaji wa wiki za hivi karibuni. Hali ambayo ilisababisha mvutano kati ya Harare na Washington. Chama tawala cha Zanu-PF kinamshtumu balozi wa Marekani kuunga mkono waasi, kufadhili machafuko nchini na kumwita 'mjinga.'

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa pia alizungumzia kitendo cha kukamatwa watu hao, na kuwataka viongozi wasitumie mapambano dhidi ya Covid-19 kukandamiza uhuru baada ya kuweka sheria ya kutotoka nje na kuchukua masharti magumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.