Pata taarifa kuu
CHAD-USALAMA-SIASA

Chad: Rais Idriss Déby afanya mabadiliko katika baraza la mawaziri

Rais wa Chad Idriss Deby amefanya mabadiliko makubwa katika serikali yake, ambapo amewateua mawaziri wapya kumi na wanne na makatibu dola sita wa serikali.

Rais wa Chad Idriss Déby katika mkutano wa kilele wa G5 Sahel, Juni 30, 2020.
Rais wa Chad Idriss Déby katika mkutano wa kilele wa G5 Sahel, Juni 30, 2020. Ludovic Marin /Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya nje imekabidhiwa Amine Abba Sidick, balozi wa sasa wa Chad nchini Ufaransa. Anachukua nafasi ya Mahamat Zene Cherif, ambaye anakuwa Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali.

Wizara mpya ya Usalama na Uhamiaji imeundwa na kukabidhiwa Mahamat Tahir Orozi, ambaye alikuwa Waziri wa Anga.

Mawaziri wa Ulinzi, Fedha na Bajeti, Uchumi, Haki na Utawala wameendelea kushikilia nafasi zao.

Hivi karibuni Wabunge wa Chad walipiga kura kwa idadi kubwa kumtunuku rais wa nchi hiyo Idriss Deby Itno cheo cha Marshal (cheo cha juu zaidi katika jeshi) kutokana na 'kazi kubwa anayoifanya kwa taifa'.

Upinzani umeendelea kulaani kitendo hicho cha wabunge wakibaini kwamba cheo hicho kinakumbusha mabaya mengi yaliyofanywa miaka ya nyuma katika historia ya Afrika.

Bunge limeptisha cheo hicho siku chache baada ya operesheni Bohoma iliyozinduliwa na jeshi la serikali dhidi ya wanamgambo wa kijihadi katika Ziwa Chad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.