Pata taarifa kuu
CHAD-SIASA-USALAMA

Rais wa Chad Idriss Déby apewa cheo cha Marshal

Wabunge wa Chad wamepiga kura kwa idadi kubwa kumtunuku rais wa nchi hiyo Idriss Deby Itno cheo cha Marshal (cheo cha juu zaidi katika jeshi) kutokana na 'kazi kubwa anayoifanya kwa taifa'.

Rais wa Chad Idriss Déby Itno wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye ikulu ya rais huko N'Djamena, Agosti 9, 2019.
Rais wa Chad Idriss Déby Itno wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye ikulu ya rais huko N'Djamena, Agosti 9, 2019. BRAHIM ADJI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Upinzani umelaani kitendo hicho cha wabunge wakibaini kwamba cheo hicho kinakumbusha mabaya mengi yaliyofanywa miaka ya nyuma katika historia ya Afrika.

Azimio hilo halikuwa kwenye ajenda, lakini Ijumaa, Juni 26, wabunge kutoka chama tawala na washirika wake walimtuku rais Idriss Deby cheo cha heshima cha Marshal, baada ya kuwa na cheo cha heshima cha Jenerali. Ametunukiwa cheo hicho kwa kazi kubwa anayoifanya kwa nchi hii, amebaini Jean-Bernard Padaré, msemaji wa chama cha MPS, chama cha rais.

"Ni cheo cha heshima, kulinganan na sheri zetu. Amepitishwa kuwa Marshal, cheo ambacho si cha jeshi, bali ni cheo cha heshima kutokana na kazi nzuri anayoifanya kwa taifa hili, " ameongeza.

Lakini kwa upande wa wabunge wa upinzani ambao walisusia kikao hicho cha bunge, cheo hicho kinakumbusha mabaya mengi yaliyopitika katika historia ya Afrika amesema Saleh Kebzabo, kiongozi wa upinzani katika bunge la Chad.

"Unaposikia cheo cha marshal, kinakufanya utabasamu, wala sio kucheka. Unaposema marshal leo barani Afrika, unafikiria Bokassa, unafikiria Idi Amine, unafikiria Mobutu, watu walioididimiza Afrika. Lakini kwa bahati mbaya kwetu, chama kilichopo madarakani kinaonyesha kwamba Chad iko katika kiwango hiki kwa sababu rais Déby, amiri jeshi mkuu, haitaji cheo kingine cha heshima. "

Hata hivyo upinzani umesema kuwa vita bado vinaendelea.

Bunge limeptisha cheo hicho siku chache baada ya operesheni Bohoma iliyozinduliwa na jeshi la serikali dhidi ya wanamgambo wa kijihadi katika Ziwa Chad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.