Pata taarifa kuu
CHAD-USALAMA

Bomu la kutegwa ardhini laua askari nane wa Chad

Wanajeshi wanane wamewauwa Magharibi mwa Chad, huku wengine kadhaa wakipata majereha baada ya gari lao kukanyaga bomu la kutegwa ardhini, lililotegwa na wapiganaji wa kijihadi.

Jeshi la Chad likipiga doria katika Jimbo la Biltine.
Jeshi la Chad likipiga doria katika Jimbo la Biltine. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka idara ya usalama nchini Nigeria, zimesema huenda idadi kamili ya wanajeshi waliopoteza maisha ikaongezeka, huku taarifa hiyo ikibaini kwamba waliotega bomu hilo ni kundi linalojiita Islamic State.

Chad ni moja ya mataifa ya Magharibi mwa Afrika ambayo yameendelea kukumbwa mashambulizi ya makundi yenye silaha, ikiwa ni pamoja na makundi ya wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali.

Rais wa Chad Idriss Deby katika mkutano wa G5 Sahel uliofanyika hivi karibuni katika mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott, alisisitiza kuwa anapendelea kuona jeshi lake linabaki nchini humo.

Wakati huo Rais wa Chad alibaini kwamba hali ya usalama si shwari nchini mwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.