Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-GBAGBO-ICC

CPI: Ombi la Laurent Gbagbo kurudi Cote d'Ivoire bado linajadiliwa

Rais wa zamani wa Côte d’Ivoire Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé ambao walifutiwa makosa yanayohusiana na uhalifu dhidi ya binadamu mwezi Januari 2019 hawako huru moja kwa moja, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, imesema katika taarifa.

Laurent Gbagbo Februari 6, 2020 mbele ya mahakama ya ICC.
Laurent Gbagbo Februari 6, 2020 mbele ya mahakama ya ICC. AFP/Jerry Lampen
Matangazo ya kibiashara

Kama Laurent Gbagbo na waziri wake wa zamani Charles Blé Goudé wanataka kuondoka katika miji wanayoishi na kwenda nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Côte d’Ivoire, wanapaswa kutoa taarifa kwa ofisi ya karani wa mahakama ya ICC imeongeza.

Siku moja baada ya uamuzi wa Mei 28 unaopunguza mazingira ya hukumu yao, Laurent Gbagbo aliiandika barua ofisi ya karani ya Mahakama ya CC na kuomba kuwa anataka kwenda nchini Côte d’Ivoire.

Kwa agizo la majaji, Karani wa Mahakama ndiye anatakiwa kujadili masharti ya kurudi nchini Côte d’Ivoire kwa rais wa zamani wa nchi hiyo, au safari zozote nje ya Ubelgiji ambapo anaishi leo.

Kwa upande wa ICC, imethibitishwa kuwa ombi hilo walilipokea na lilitumwa kwa mamlaka nchini Côte d’Ivoire. Chanzo kingine kimesema kwamba ombi hilo lilitumwa Juni 10.

Kwa muda wa wiki tatu, mamlaka nchini Côte d’Ivoire hawajathibitisha wala kupinga kuwa wamepokea ombi hilo.

Wakati wa kesi ya rais huyo wa zamani wa Côte d’Ivoire mjini Hague mwenzi Februari, wanasheria wa Côte d’Ivoire walipinga kurudi kwa Laurent Gbagbo nchini humo, wakisema wana hofu ya kutokea machafuko nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.