Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-GBAGBO-MAZUNGUMZO-SIASA

Uchaguzi wa urais Côte d’Ivoire: Rais wa zamani Laurent Gbagbo atoa wito wa mazungumzo ya amani

Rais wa zamani wa Côte d’Ivoire Laurent Gbagbo, ametoa wito wa kuepo kwa mazungumzo wakati nchi hii ikijiandalia Uchaguzi Mkuu, wakati huu muhula wa Alassane Ouattara ukikaribia kufikia ukingoni.

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo, Januari 28, 2016, wakati akisikilizwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ay Jinai huko Hague, Uholanzi. (Picha kumbukumbu)
Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo, Januari 28, 2016, wakati akisikilizwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ay Jinai huko Hague, Uholanzi. (Picha kumbukumbu) ICC-CPI
Matangazo ya kibiashara

Kwa miaka ishirini, kila uchaguzi nchini Cote d'Ivoire umekuwa ukikumbwa na vurugu zinazohusiana na uchaguzi. Na kuna ishara kwamba hali kama hiyo inaweza kutoke, ameonya Laurent Gbagbo katika taarifa.

Rais Gbagbo amewataka wanasiasa, lakini pia viongozi wa kidini pamoja na mashirika ya kiraia kufanya mazungumzo ili kujifunza kile kilichotokea.

Kile ambacho hatupaswi kusahau pia kuwa bado tuna majeraha yaliyotokea mwaka 2010 na ni muhimu kwamba tunaweza kuondoa majeraha haya, maumivu haya.

Hivi karibuni Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC, ilisema rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé wanaweza kuondoka nchini Ubelgiji na Hague chini ya masharti.

Msemaji wa Mahakama hiyo alisema Gbagbo mwenye umri wa miaka 73 yuko huru na anaweza kwenda katika taifa analotaka iwapo taifa hilo litamruhusu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.