Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-ICC-GBAGBO-HAKI

ICC yatathmini ombi la kesi ya rufaa dhidi ya Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé wamefikishwa tena mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai huko Hague Jumatatu hii, Juni 22.

Waziri wa zamani wa Vijana nchini Cote d'Ivoire Charles Blé Goudé (kushoto) na rais wa zamani Laurent Gbagbo (kulia), katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC huko Hague.
Waziri wa zamani wa Vijana nchini Cote d'Ivoire Charles Blé Goudé (kushoto) na rais wa zamani Laurent Gbagbo (kulia), katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC huko Hague. Peter Dejong / POOL / AFP/ Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Wawili hawa wanasikilizwa mbele ya kitengo cha Rufaa cha Mahakama hiyo ya Kimataiafa, ICC, kufuatia hatua ya Mwendesha mashtaka Fatou Bensouda ya kukata rufaa dhidi ya kufutiwa makosa yanayohusiana na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, uamuzi uliochukuliwa na ICC mwishoni mwa mwezi Januari 2019.

Mwaka mmoja na nusu baada ya uamuzi wa kuachiliwa huru, hii awamu mpya katika kesi ya Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé mbele ya ICC. Mwanzoni, mwendesha mashtaka alionyesha mashahidi 82 mbele ya majaji wa ICC, na kutoa ushahidi kuhusu kuhusika kwa Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé katika machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 na 2011.

Wakati huo Majaji walichukua uamuzi wa kuwaachilia huru wawaili hao na kuonyesha "udhaifu wa kipekee" katika ushahidi uliotolewa na mwendesha mashtaka. Baada ya uamuzi huo Fatou Bensouda alikataa rufaa.

Lengo ni "kuona ikiwa uamuzi wa kuachiliwa huru unaweza kuthibitishwa, au ikiwa kesi hiyo inaweza tena kurejelewa, ili mwendesha mashtaka aitishwe kuonyesha ushahidi," Fadi El Abdallah, msemaji wa ICC amesema.

Fatou Bensouda amebaini kwamba makosa ya kisheria yalifanyika wakati wa kupitishwa uamuzi wa kuachiliwa huru Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.